Pata taarifa kuu
MAREKANI

Mwaka mmoja baada ya Trump, NBA yarudi White House

Katika kipindi chote cha uongozi wa Trump, timu za NBA zilizoshinda ubingwa wa Marekani zilisusia kuingia katika Ikulu ya White House, nchini Marekani. Uhasama ambao Joe Biden amemaliza.

Novemba 8, 2021; Washington, DC, Marekani; Rais wa Marekani Joe Biden akiwakaribisha Milwaukee Bucks katika Ikulu ya White House  ili kupongeza timu hiyo kwa ubingwa wake wa NBA.
Novemba 8, 2021; Washington, DC, Marekani; Rais wa Marekani Joe Biden akiwakaribisha Milwaukee Bucks katika Ikulu ya White House ili kupongeza timu hiyo kwa ubingwa wake wa NBA. USA TODAY Sports - Scott Taetsch
Matangazo ya kibiashara

Mpira wa kikapu wa kiwango cha juu umerejea katika Ikulu ya White House, miaka mitano baada ya kususa. Jumatatu, Novemba 8, Joe Biden aliwakaribisha wachezaji na makada wa Milwaukee Bucks, washindi wa NBA mwezi Julai 2021. Kwa kukubali mwaliko wa rais kutoka chama cha Demokratic, wachezaji wa mpira wa kikapu wa Milwaukee wamerudi kwenye utamaduni ambao unataka rais wa Marekani kupokea timu bingwa kila mwaka.

Wakati wote wa uongozi wa Trump, timu zilizoshinda taji la matoleo ya 2016 hadi 2020 zilikataa kuitikia mwaliko wa timu za rais kutoka chama cha Republican, hasa kwa kupinga wazo walilo nalo la sera ya Donald Trump kuhusu jamii za walio wachache.

Siku ya Jumatatu, wachezaji na makocha wa Milwaukee walikutana na ras Joe Biden, ambaye alimsifu Donte DiVincenzo, ambaye wanatoka jimbo moja la Delaware.

Joe Biden pia alipongeza mfungaji bora wa Bucks Giannis Antetokounmpo ambaye ametoka kwenye umaskini nchini Ugiriki, ambapo alikuwa akivaa viatu na kaka yake, ili kutimiza ndoto ya Marekani. "Niliguswa kidogo," alijibu Antetokounmpo, "Ninajua jinsi (familia yangu) ilijitolea,, ni muda mrefu tangu nilipokuwa mtoto."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.