Pata taarifa kuu
MAREKANI-HAKI

Mashambulizi dhidi ya Capitol: Kamati ya bunge kuwasikiliza wasaidizi wa Trump

Kamati maalum ya Baraza la Wawakilishi imewaitisha wasaidizi sita wa rais wa zamani wa Marekani Donald Trumpili kuja kutoa ushahidi katika uchunguzi wa bunge kuhusu shambulio la Capitol Hill ambalo lilifanyika Januari 6.

Kamati maalum inawaangalia washauri wa Donald Trump ambao walidai kuwa uchaguzi wa Joe Biden ulijawa na udanganyifu au ambao walijitahidi kutafuta njia ya kutengua matokeo ya uchaguzi.
Kamati maalum inawaangalia washauri wa Donald Trump ambao walidai kuwa uchaguzi wa Joe Biden ulijawa na udanganyifu au ambao walijitahidi kutafuta njia ya kutengua matokeo ya uchaguzi. Sarah Silbiger GETTY IMAGES NORTH AMERICA/AFP/Archivos
Matangazo ya kibiashara

Wajumbe tisa wa tume hiyo maalum wamesema mara kadhaa kwamba wanakusudia kuona kesi hiyo ikimalizika, baada ya uchunguzi wao kuhusu shambulio la Januari 6 kukamilika.

Katika kuitishwa huku, wamekusudia hasa washauri wa Donald Trump ambao walidai kuwa uchaguzi wa Joe Biden ulijawa na udanganyifu au ambao walijitahidi kutafuta njia ya kutengua matokeo.

Kambi ya Trump bado iko kimya

Bill Stepien, meneja wa kampeni wa Donald Trump au mshauri wake wa zamani wa usalama wa kitaifa Michael Flynn ni miongoni mwa watu hao sita. Wanaombwa kutoa hati kabla ya mwisho wa mwezi huu na kujibu maswali kutoka kwa kamati mwanzoni mwa mwezi Desemba. Mwitikio wao utakuwa wa kuvutia. Labda watasubiri kujua kitakachowapata wale walioitishwa kwa mara ya kwanza.

Kambi ya Trump hadi sasa haijaonesha nia yoyote ya kushirikiana na tume hiyo. Aliyekuwa mshauri wa kisiasa Steve Bannon alikataa kuitikia wito huo na sasa anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu. Kuhusu rais huyo wa zamani, alimwomba jaji azuie kuwasilishwa kwa hati zilizoombwa na tume hiyo na kuziweka katika maktaba ya kitaifa kuhusu hati za serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.