Pata taarifa kuu
MAREKANI-HAKI

Marekani: Maafisa wa polisi wahusishwa katika vurugu za Capitol Hill

Mmoja wa afisa wa Polisi aliyekuwa analinda eneo la Capitol Hill jijini Washington DC nchini Marekani, makao makuu ya bunge amesema alihofia huenda angeuliwa na waandamanaji waliokuwa wanamuunga mkono rais wa zamani Donald Trump

Maafisa wa polisi waliokuwepo wakati wa shambulio la Capitol walitoa ushuhuda wao kuhusu uvamizi huo mbele ya tume ya pande mbili iliyoundwa Julai 27, 2021 huko Washington.
Maafisa wa polisi waliokuwepo wakati wa shambulio la Capitol walitoa ushuhuda wao kuhusu uvamizi huo mbele ya tume ya pande mbili iliyoundwa Julai 27, 2021 huko Washington. © Oliver Contreras/AP
Matangazo ya kibiashara

Maandamano hayo yalishuhudiwa Januari 6 wakati waandamanaji hao walipovamia majengo ya bunge kudai wizi wa kura.

Afisa huyo Aquilino Gonell ameilezea Kamati ya Congress inayochunguza maandamano na vurugu hizo hali ilivyokuwa.

Machafuko tuliyoshuhudia yalikuwa mabaya sana, maafisa wenzangu pamoja na mimi, tulipiwa makonde, tukapigwa mateke na kunyunyuziwa kemikali yenye sumu, yenye kupofusha lakini cha ajabu tuliendelea na kazi ya kuwalinda kama raia wa Marekani walipojaribu kuingia kwenye majengo ya bunge, mimi nilipigwa sana na waandamanaji na nikajiambia hivi ndivyo nitakavyopoteza maisha, nikilinda lango hili.

Waandamanaji zaidi ya 500 walikamatwa na kusababisha vifo vya watu watano, akiwemo afisa mmoja wa polisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.