Pata taarifa kuu
MAREKANI-UCHUNGUZI

shambulio Capitol: Ivanka Trump alimuomba babake Donald Trump kutuliza wafuasi wake

Ili kutoa mwanga kuhusu shambulio dhidi ya makao makuu ya Bunge nchini Marekani, Capitol Hill, na umati wa wafuasi wanaomuunga mkono Trump, Januari 6, 2021, tume ya uchunguzi imeundwa na Baraza la Wawakilishi.

Ivanka Trump, binti wa Donald Trump, hapa akiwa na baba yake.
Ivanka Trump, binti wa Donald Trump, hapa akiwa na baba yake. AP - Pablo Martinez Monsivais
Matangazo ya kibiashara

Wabunge wawili pekee kutoka chama cha Republican ndio wanashiriki katika shughuli hii ya tume, akiwemo Liz Cheney ambaye alifichua Jumapili, Januari 2 kuwa na ushuhuda muhimu kuhusu tabia ya rais Donald Trump siku hiyo ya vurugu katika makao makuu ya Bunge.

Kulingana na Liz Cheney, tume ya uchunguzi ina ushahidi kwamba Ivanka Trump, bintiye na mshauri wa rais wa zamani, alimwomba babake kuingilia kati wakati wa shambulio la Capitol Hill. Lakini Donald Trump aliendelea kutazama matukio hayo moja kwa moja kwenye runinga kwenye sebule yake ya kibinafsi.

Liz Cheney hakusema alipata wapi habari hii. Ivanka Trump sio pekee aliyemwomba babake kuzungumza ili kutuliza umati, kulingana na Tume ya Uchunguzi. Mwanawe, Donald Trump Jr., pia alijaribu kumuomba babake, pamoja na kiongozi wa chama cha Republican katika Bunge hilo kuingilia kati, bila mafanikio. Ni baada ya shambulio hilo ambapo rais hatimaye alihutubia wafuasi wake, katika video fupi iliyowekwa kwenye mtandao wa Twitter, akiwataka warudi nyumbani.

Kufikia sasa, tume ya uchunguzi imewahoji karibu watu 300. Tatizo ni kwamba wafuasi wengi wa rais huyo wa zamani wanakataa kutoa ushirikiano. Ripoti ya kwanza inatarajiwa msimu ujao wa joto. Na muda kwa tume hiyo unazidi kukimbia: ikiwa Warepublican wataidhibiti tena Ikulu wakati wa uchaguzi wa katikati ya muhula ujao wa mwezi Novemba, bila shaka watasitisha shughuli hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.