Pata taarifa kuu
MAREKANI-HAKI

Trump hatarini kuhusishwa na shambulio dhidi ya Capitol Hill

Mahakama ya rufaa nchini Marekani imedhinisha Braza la Congress kukabidhiwa hati ambazo zinaweza kumhusisha Donald Trump na shambulio la Januari 6 kwenye makao makuu ya Bunge la Capitol Hill, kikwazo kwa rais huyo wa zamani ambaye anataka kuendelea mbele.

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump kabla ya kupanda jukwaani katika mkutano wa kampeni za uchaguzi wa Septemba 25, 2021 huko Perry, Georgia.
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump kabla ya kupanda jukwaani katika mkutano wa kampeni za uchaguzi wa Septemba 25, 2021 huko Perry, Georgia. AP - Ben Gray
Matangazo ya kibiashara

Hiki ni kikwazo cha pili cha kisheria kwa rais huyo wa zamani. Majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa wanathibitisha uamuzi uliochukuliwa katika mahakama ya mwanzo. Kulingana na majaji hao, Donald Trump hana uwezo wa kuzuia hati inazohitaji kamati maalum ya Baraza la Wawakilishi, ameripoti mwandishi wetu wa Washington, Guillaume Naudin.

Bilionea huyo anasema ni haki yake kama mtu mwenye hadhi aliye wahi kuongoza Marekani. Kulingana na majaji hao, haki hii si ya marais wa zamani, bali ya rais aliyepo madarakani. Na Joe Biden ameonyesha nia yake ya kusambaza kurasa 800 za hati hizo, kumbukumbu za wageni, barua pepe, rasimu ya hotuba na madokezo. Ni sawa kwa mujibu wa majaji wanaoeleza kuwa usiri hauko kwa maslahi ya taifa kutokana na uzito wa kilichotokea Januari 6.

Uamuzi huu unafungua njia ya kutumwa kwa mamia ya kurasa za hati kwa tume ya bunge iliyoshtakiwa kwa kutoa mwanga juu ya jukumu la rais wa zamani kutoka chama cha Republican katika shambulio hili.

Wiki mbili za kukata rufaa

Hii haimaanishi kwamba hati zitatumwa mara moja kwa kamati maalum. Mawakili wa Donald Trump wana wiki mbili kuiomba Mahakama ya Juu kutoa uamuzi wa dharura. Hukumu yake itakuwa ya kuvutia kutoka kwa mtazamo wa kisheria, kwa hakika hakuna sheria ya kesi juu ya upeo wa upendeleo wa serikali. Lakini pia kisiasa.

Mwenyekiti wa tume hiyo, Mdemokrat aliyechaguliwa Bennie Thompson, na naibu wake wa kutoka chama cha Republican Liz Cheney wamekaribisha uamuzi wa mahakama. "Tutafikia ukweli," walisema katika taarifa. Spika wa Baraza la Wawakilishi kutoka chama cha Democratic Nancy Pelosi, pia amekaribisha uamuzi huo, akisema "hakuna mtu anayepaswa kuruhusiwa kuzuia njia inayotafuta ukweli".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.