Pata taarifa kuu

Venezuela: mfumo wa afya wakumbwa na hali tete baada ya hali ya maisha kuzorota

Raia wa Venezuela wametakiwa kupiga kura Jumapili hii, Novemba 21 kuwachagua magavana na wabunge wa majimbo 23 ya nchi hiyo pamoja na mameya. Lakini hali duni ya maisha inawalazimu raia kujitenga na siasa.

Afya ya raia wa Venezuela inazidi kuzorota. Hapa, mtoto anapokea dozi wakati wa kampeni ya chanjo ya Corona huko Caracas, Oktoba 27, 2021.
Afya ya raia wa Venezuela inazidi kuzorota. Hapa, mtoto anapokea dozi wakati wa kampeni ya chanjo ya Corona huko Caracas, Oktoba 27, 2021. REUTERS - LEONARDO FERNANDEZ VILORIA
Matangazo ya kibiashara

Kwa upande mwingine, wana athari ya moja kwa moja kwa afya. Mkurugenzi wa Kituo cha Uangalizi wa Afya cha Venezuela anapaza sauti kwa mara nyingine tena ili mfumo wa afya nchini Venezuela uweze kushughulikiwa.

Kwa mara ya kwanza baada ya miaka mitatu, upinzani unashiriki katika uchaguzi wa Jumapili hii. Lakini Wavenezuela wengi wameamua kujitenga na siasa. Wengi wanajihusisha na maisha yao ya kila siku.

Kwa upande wa Marianella Herrera Cuenca, mkurugenzi wa Kitengo cha Uangalizi wa Afya nchini Venezuela, na wenzake wanasema hakuna shaka: sababu kuu ya kuzorota kwa afya nchini Venezuela ni ukosefu wa chakula. "Asilimia 91 ya wananchi wa Venezuela leo wanakabiliwa na aina fulani ya uhaba wa chakula. Ukosefu wa lishe unaongezeka kwa raia kwa ujumla. Matokeo ya hali hii ni kudhoofika kwa kinga ya mwili, kuhara au hata kupatawa na ugonjwa wa nimonia. Na yote haya yanahatarisha hali ya afya, "ameongeza.

Mfumo wa hospitali ya umma hatarini

Sababu ya pili ambayo inazidisha matatizo ya kiafya ya Wavenezuela ni mfumo duni wa hospitali za umma.

Lakini kinachomtia wasiwasi mkurugenzi wa kitengo cha Uangalizi wa Afya nchini Venezuela ni kwamba nchi hiyo "inarudi nyuma katika sayansi." "Na hiyo ni mbaya! Hatuna maendeleo yoyote ya hivi punde ya kisayansi ambayo yataturuhusu kuwatibu wagonjwa wetu. Chukulia mfano wa wagonjwa wa saratani kwa vijana wa kiume: katika nchi nyingine, wanapona bila tatizo lolote, hapa watakufa tu,” amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.