Pata taarifa kuu
VENEZUELA-SIASA

Venezuela: Duru mpya ya mazungumzo ya kisiasa kuanza Ijumaa

Duru mpya ya mazungumzo kati ya wawakilishi wa serikali ya Nicolás Maduro na upinzani nchini Venezuela inaaza Ijumaa hii Septemba 24 huko Mexico. Baada ya mikutano miwili ya kwanza mwezi Agosti na mapema mwezi Septemba, pande hizo mbili zitajaribu kusonga mbele kufikia makubaliano kamili ambayo yatawezesha Venezuela kuwa na mustakabali mzuri na kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa huru na haki.

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro.
Rais wa Venezuela Nicolas Maduro. Yuri CORTEZ AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Ni mazungumzo ambayo hufanyika chini ya mwavuli wa Norway, na ambayo hata Washington inaona yatazaa matunda, wakati serikali ya Marekani haitambui uhalali wa rais Maduro kama mkuu wa Venezuela.

Chini ya mwezi mmoja baada ya "duru" ya pili ya mazunumzo, ambayo yalifanya iwezekane kutia saini kwenye makubaliano juu ya pointi mbili, upinzani nchini Venezuela na wawakilishi wa serikali ya Nicolás Maduro watakutana tena katika Jiji la Mexico kwa siku nne za mazungumzo, kuanzia Ijumaa hii .

Na ikiwa mwezi mmoja uliopita hakukuwa na uharaka, sasa uchaguzi ujao wa serikali za mitaa na wa mkoa unaotarajiwa kufanyika chini ya kipindi cha miezi miwili, ni muhimu kufikia suluhisho.

Wakati upande wa maafisa wa serikali wanaona kuondolewa kwa vikwazo vya kiuchumi vilivyowekwa dhidi ya Venezuela bado ni sharti la makubaliano ya mwisho, upinzani hauioni hivyo, ukitoa wito kwa kufanyika kwa uchaguzi huru na wazi kabla ya kuondolewa kwa vikwazo.

Kwa hivyo kuna hatari kwamba duru hii mpya haitafaulu. Lakini kama Mku wa sera za Mambo ya Nje wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell alivyoeleza wiki hii, ikiwa mazungumzo haya yatafanikiwa, hakutakuwa na tija ya kuweka vikwazo.

Norway na Mexico, ndio kama wadhamini wa mazungumzo haya, kwa hivyo watalazimika kushawishi. Hasa kwa kuwa wakati unapita, ndivyo hali ya chakula, afya, kijamii na kiuchumi inavyozidi kuwa mbaya katika nchi ambayo tayari inaendelea kukabiliwa na hali nzito.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.