Pata taarifa kuu
VENEZUELA-UCHUMI

Venezuela: wakazi watatu kati ya wanne wanaishi katika umaskini uliokithiri

Sarafu ya Venezuela iko hatarini kupoteza thamani, Ijumaa hii, Oktoba 1. Tangu mwaka 2008, zero kumi na nne zimefutwa. Kuporomoka huku huu kwa sarafu ya Venezuela unaenda sambamba na jambo lingine: umaskini uliokithiri wa unaowakabili raia wa nchi hiyo.

Wakazi watatu kati ya wanne wanaishi katika umasikini uliokithiri nchini Venezuela, ambayo iinakabiliwa na mgogoro wa kiuchumi usiyo na kifani.
Wakazi watatu kati ya wanne wanaishi katika umasikini uliokithiri nchini Venezuela, ambayo iinakabiliwa na mgogoro wa kiuchumi usiyo na kifani. © AP - Ariana Cubillos
Matangazo ya kibiashara

Leo, zaidi ya watu tisa kati ya kumi nchini Venezuela ni maskini. Zaidi ya watatu kati ya wanne nchini Venezuela wanaishi chini ya kiwango cha umaskini uliokithiri. Haya ni matokeo ya uchunguzi wa hivi karibuni katika ngazi ya kitaifa juu ya hali ya maisha, uliyotolewa Jumatano hii na Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Andrés Bello huko Caracas.

Ni miaka minane sasa uchumi wa Venezuela ukidorora. Mfumuko wa bei, kushuka kabisa kwa uzalishaji karika ngazi ya kitaifa na uhaba wa kila aina ya bidhaa vimesababisha watu kuwa katika maisha magumu. Lakini hali hii imechochewa zaidi na janga la Covid-19 na hasa uhaba wa petroli ambayo  taifa hili lenye mafuta ambayo yamekosekana.

Wavenezuela ambao bado walmekuwa na kazi wamelazimika kuachana nayo. Kwa sababu usafiri unawagharimu zaidi ya mshahara wanaoweza kupata. Leo, zaidi ya nusu ya Wavenezuela wa umri wa kufanya kazi hawana kazi. Ukosefu wa ajira unaathiri wanawake wawili kati ya watatu.

Kima cha chini cha mshahara huongezewa na malipo ya serikali

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.