Pata taarifa kuu
MEXICO

Kuzuia mwanamke kutoa mimba ni kinyume cha katiba Mexico

Mahakama Kuu ya Mexico imeamua kuwa uhalifu wa utoaji mimba ni kinyume cha Katiba, kwa kura ya pamoja Jumanne, uamuzi ambao utawawezesha wanawake wa Mexico kote nchini kutoa mimba bila kizuizi.

Chanzo cha kimahakama kimeeleza kwamba uamuzi huu kwa kweli una upeo wa kitaifa kwa sababu utawaruhusu wanawake ambao wanaishi katika majimbo ambayo utoaji wa mimba ni uhalifu kutoa mimba kwa uamuzi wa jaji.
Chanzo cha kimahakama kimeeleza kwamba uamuzi huu kwa kweli una upeo wa kitaifa kwa sababu utawaruhusu wanawake ambao wanaishi katika majimbo ambayo utoaji wa mimba ni uhalifu kutoa mimba kwa uamuzi wa jaji. AFP - ALFREDO ESTRELLA
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huu umeelezewa kama "wa kihistoria" na watetezi wa haki za binadamu katika nchi hii ya kihafidhina yenye waumini wengi wa kanisa Katoliki huko Amerika Kusini.

- "Kwa usawa, na utu" -

"Hii ni hatua moja zaidi katika mapambano ya kihistoria ya usawa (wa wanawake), utu na utekelezaji kamili wa haki zao," ametangaza mkuu wa Mahakama hiyo, Arturo Zaldivar.

"Kuanzia sasa haitawezekana, bila kukiuka vigezo vya mahakama na Katiba, kumshtaki mwanamke anayetoa mimba katika kesi zilizoidhinishwa na mahakama hii", ameeleza Arturo Zaldívar.

Mahakama hii ilikutana kwa siku mbili ili kujadili uhalali wa Ibara za kanuni za jukumu la jinai za jimbo la Coahuila, kaskazini mwa Mexico, ambazo zinawaadhibu wanawake wanaotoa mimba, hadi kifungo cha miaka mitatu jela.

Ibara hizi zilipitishwa kwa kauli moja kuwa ni kinyume cha katiba na majaji kumi walioshiriki kikao hiki.

Chanzo cha kimahakama kimeeleza kwamba uamuzi huu kwa kweli una upeo wa kitaifa kwa sababu utawaruhusu wanawake ambao wanaishi katika majimbo ambayo utoaji wa mimba ni uhalifu kutoa mimba kwa uamuzi wa jaji.

"Mwanamke lazima aombe (huduma za afya) atoe mimba, na ikiwa watakataa kufanya hivyo, anaweza kwenda mahakamani na kutoa malalamiko yake. Jaji sasa atakuwa na uwezo wa kuagiza utoaji mimba," Alex Alí Méndez, wakili wa kikatiba na mtaalam wa masuala ya utoaji mimba, ameliambia shirika la habarila AFP.

Uamuzi wa Mahakama Kuu, wakili huyo ameongeza, utapelekea wanawake waliofungwa kwa kosa la kutoa mimba kuaciliwa huru.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.