Pata taarifa kuu
MEXICO

Kimbunga Grace chakaribia Mexico, raia waonywa kuhamia maeneo salama

Kimbunga Grace kinaendelea kuathiri maeneo kadhaa katika bara la Amerka na kimezidisha kasi usiku wa Ijumaa kuamkia leo Jumamosi kabla ya kupiga Mexico kwa mara ya pili, ambapo maonyo ya mafuriko na maporomoko ya ardhi yametolewa.

Watu hukusanyika karibu na miti iliyoangushwa baada ya Kimbunga Grace kupiga kwenye Rasi ya Yucatan, huko Tulum, Mexico, Agosti 19, 2021.
Watu hukusanyika karibu na miti iliyoangushwa baada ya Kimbunga Grace kupiga kwenye Rasi ya Yucatan, huko Tulum, Mexico, Agosti 19, 2021. REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Jumamosi saa 09:00 usiku saa za kimataifa, kimbunga Grace kilionekana kilomita 120 kutoka Tuxpan, katika jimbo la Veracruz, mashariki mwa Mexico, kikiambataka na upepo mkali uliokuwa ukivuma kwa kasi ya kilomita 195 kwa saa, kulingana na Kituo cha Marekani kinachoshughulika na masuala ya vimbunga (NHC).

"Grace kimekuwa kimbunga hatari," kilichowekwa katika kiwango cha 3, kimesema kituo cha NHC, ambacho awali kilitangaza kwamba kimbunga hicho kiko katika kiwango cha 2. Taasisi hiyo haiondoi uwezekano wa kuwa kimbunga hicho kitazidi kushika kasi kabla ya kutulia usiku.

Kimbunga hicho "kitaathiri saa chache zijazo pwani ya kaskazini ya Veracruz, karibu na manispaa ya Tecolutla", imeonya mamlaka ya Maji ya Mexico kwenye mitandao ya kijamii. Ni sehemu ya kaskazini ya jimbo hili ambayo inapaswa kuathiriwa zaidi, kwa sehemu kubwa ya pwani.

Kimbunga Grace kinaweza kuharibu nyumba na majengo ya pwani, kusomba miti na mabango barbarani na kusababisha mafuriko katika maeneo ya pwani, mamlaka ya maki imeongeza.

Wakati kitakuwa kikipita sehemu za chini, kimbunga hicho kinatabiriwa kuwa kitaanza kupoteza nguvu, hasa kitapogonga milima. Walakini, jimbo la Veracruz lina mito mingi yenye nguvu, ambayo huiweka mamlaka kwenye tahadhari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.