Pata taarifa kuu
MEXICO-COVID 19

Idadi ya vifo Mexico yazidi idadi ya vifo India

Mexico imerekodi visa vipya 18,670 vilivyothibitishwa vya maambukizi ya virusi vya Corona na vifo 1,506 vipya vilivyotokana na janga hilo katika muda wa saa ishirini na nne zilizopita, kulingana na takwimu zilizoripotiwa na Wizara ya Afya.

Rais wa Mexico wakiwa wamevalia barakoa kujikinga na janga la Corona
Rais wa Mexico wakiwa wamevalia barakoa kujikinga na janga la Corona REUTERS/Carlos Jasso
Matangazo ya kibiashara

Hii inafanya visa vya maambukizia ukufikia 1,825,519 na vifo 155,145 tangu kuzuka kwa janga hilo, takwimu za serikali zinaonyesha.

Idadi ya watu ambao wamefariki duni kutokana na COVID-19 nchini Mexico sasa inazidi ile ya India, kulingana na hesabu iliyotolewa na shirika la habari la REUTERS,.

Hali hiyo sasa inaifanya nchi hiyo ya Amerika ya Kati kuwa ya tatu iliyoathiriwa zaidi na mgogoro wa kiafya ulimwenguni kwa vifo, baada ya Marekani na Brazil.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.