Pata taarifa kuu
MAREKANI-USHIRIKIANO

Afghanistan: Joe Biden atetea hatua yake ya kuondoa vikosi vya Marekani

Katika hotuba yake, Jumatatu, Agosti 16, Rais wa Marekani alikiri kuchukua uamuzi wa kuondoa wanajeshi kutoka Afghanistan, nchi ambayo imeanguka mikononi mwa Taliban. 

Rais wa Marekani Joe Biden Agosti 16, 2021 katika Ikulu ya White House, Washington.
Rais wa Marekani Joe Biden Agosti 16, 2021 katika Ikulu ya White House, Washington. AP - Evan Vucci
Matangazo ya kibiashara

Kuanguka huku kulitokea "haraka" kuliko vile alivyotarajia. Lakini Joe Biden anaamini kwamba wananchi wa Afghanistan walishindwa "kuamua hatima ya taifa lao". Na amesema nchi yake iko tayari kuingilia kijeshi dhidi ya Taliban "ikiwa itahitajika".

Saa chache baada ya rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kulihutubia taifa, rais wa Marekani Joe Biden naye, alilihutubia taifa Jumatatu kuhusiana na hali nchini Afghanistan, ambapo Taliban ilirejesha tena madaraka mikononi mwake ka kipindi kifupi, baada ya miaka zaidi ya ishirini kutimuliwa na muungano wa vikosi vya kimataifa.

Rais wa Marekani Joe Biden anakabiliwa na ukosoaji mkubwa kutoka ndani na nje ya nchi hiyo kutokana na hatua ya haraka ya kuondoa vikosi vya Marekani nchini Afghanistan.

Hata hivyo, Joe Biden "ametetea wazi" hatua yake ya kuondoa vikosi vya Marekani nchini Afghanistan. "Baada ya miaka 20, nimeona hakuna umuhimu vikosivyetu kuendelea kubaki nchini Afghanistan," amesema. Na kuongeza kuwa: "Lengo letu huko Afghanistan haikuwa kamwe kujenga taifa" Lengo la Marekani lilikuwa "kuzuia shambulio la kigaidi kwenye ardhi ya Marekani", baada ya matukio ya Septemba 11, 2001.

Wanachi wa Afghanistan walishindwa "kuamua hatima ya taifa lao", Biden amebaini.

Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani wakati alipokimbilia mafichoni, Taliban haraka ilichukuwa udhibiti wa nchi. Afghanistan ilianguka mikononi mwao "haraka kuliko ilivyotarajiwa", amekiri rais wa Marekani, ambaye analinyooshea kidole cha lawam jeshi la Afghanistan: kulingana rais Joe Bideni, Marekani imewapa wanajeshi wa Afghanistan "chaguzi zote za kuamua hatima ya taifa lao" na kuikabili vilivyo Taliban. "Vikosi vya Marekani haviwezi, na havipaswi, kuendesha vita na kupoteza maisha kwa vita visivyowahusu wakati vikosi vya Afghanistan havitaki kupigania taifa lao," amesema rais wa Marekani.

Mwisho wa hotuba yake, Joe Biden aliondoka bila kujibu maswali ya waandishi wa habari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.