Pata taarifa kuu
MAREKANI-URUSI

Mshauri wa zamani wa Trump akiri kuidanganya FBI kuhusu mawasiliano yake na Urusi

Mshauri wa zamani wa rais wa Marekani Donald Trump, Michael Flynn, amekiri kulidanganya shirika la ujasusi la Marekani FBI kuhusu mawasiliano yake na Urusi,katika hatua ya kuongezeka kwa kasi kwa uchunguzi dhidi ya madai ya kuwepo kwa ushirikiano kati ya timu ya kampeni ya rais Trump na Moscow.

Mshauri wa zamani wa rais Trump, Michael Flynn
Mshauri wa zamani wa rais Trump, Michael Flynn REUTERS/Carlos Barria
Matangazo ya kibiashara

Flynn mwenye umri wa miaka 58 generali mstaafu wa jeshi mwenye nyota tatu, ni mhusika mkuu zaidi aliyepatikana na hatia katika uchunguzi maalum wa mwendesha mashitaka Robert Mueller katika madai ya Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani mwaka jana.

Flynn alifika mahakamani jana Ijumaa kabla ya kufanyika kwa kikao cha mahakama Ijumaa asubuhi mjini Washington DC na kukiri kosa moja la kutoa taarifa za uongo, za kubuni na za kupotosha kwa makusudi kwa shirika la ujasusi FBI.

Kwa mujibu wa mwanahabari wa AFP, Bw Flynn aliulizwa na Jaji Rudolph Contreras iwapo alitaka kukiri makosa hayo na akajibu kwa kusema ndio kisha jaji akasema anakubali kukiri kwake na hivyo hakutakuwa na kusikizwa kwa kesi na labda huenda kusiwe na rufaa.

Mnamo Oktoba, meneja wa zamani wa kampeni za urais wa Trump, Paul Manafort, alituhumiwa kula njama ya kuilaghai Marekani katika shughuli za kibiashara na Ukraine.

Aidha, iliibuka kwamba msaidizi mwingine wa zamani, George Papadopoulos, amekiri makosa ya kutoa taarifa za uongo kwa maajenti wa FBI.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.