Pata taarifa kuu
MAREKANI-OBAMACARE-AFYA

Trump: Republican watapata kura nyingi za kufuta Obamacare

Donald Trump amesema Jumatano hii kuwa Republican watakuwa na kura za kutosha kwa kufuta sheria ya bima ya afya iliyopitishwa chini ya utawala wa Barack Obama, lakini kabla ya muda wa mwisho wa Septemba 30.

Waandamanaji wa Tea Party,  Septemba 10, wakiandamana dhidi ya mageuzi mfumo wa huduma ya Afya kwa bei nafuu uliyowekwa na utawala wa Barack Obama"Obamacare,"  Washington.
Waandamanaji wa Tea Party, Septemba 10, wakiandamana dhidi ya mageuzi mfumo wa huduma ya Afya kwa bei nafuu uliyowekwa na utawala wa Barack Obama"Obamacare," Washington. REUTERS/Jonathan Ernst
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani amesema hayo katika tweet siku moja baada ya kushindwa kwa jaribio jipya la Grand Old Party la kufuta Obamacare, kwa kukosa idadi kubwa katika baraza la Seneti.

"Tutakuwa na kura nyingi kwa kufuta bima ya afya ya Obamacare lakini kabla ya tarehe ya mwisho ya maridhiano siku ya Ijumaa," amesema Donald Trump. Amesema hiyo ni "ishara nzuri sana" zilizotumwa na wabunge kadhaa, ambao hakuwataja.

Chama cha Republican, ambacho kina viti vidogo, 52 dhidi ya 48 katika baraza la Seneti, kina muda hadi kufikia Septemba 30 kuwa kimepitisha nakala yao inayorejelea Sheria ya huduma ya afya ya kwa wingi wa kura wa kawaida, badala ya kura 60 zinazohitajika katika baraza la Seneti.

Siku ya Jumanne, viongozi kadhaa wa chama cha Republican walisema juhudi zao sasa zinaelekea kwenye mageuzi ya kodi yaliyotakiwa na Donald Trump.

Seneta wa Republican Rand Paul, ambaye kwa muda mrefu alitetea kukamilika kwa Obamacare, amesema chama chake kinaweza kurekebisha bima ya afya wakati wowote ingawa sasa tahadhari inalenga mageuzi ya kodi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.