Pata taarifa kuu

Watu walioendesha shambulio dhidi kambi ya jeshi waendelea kukamatwa Venezuela

Mamlaka Venezuela imeendelea kuwakamata wahusika wa "shambulio la kigaidi" dhidi kambi ya jeshi katika mji wa Valencia, kaskazini ya nchi hiyo na kujaribu kutoa wito kwa "umoja" wa jeshi ili kuepuka mtafaruku.

Vikosi vya ulinzi na usalama vikiendelea kuwasaka wati waliohusika na shambulio dhidi ya kambi ya jesi ya Paramacay, nchini Venezuela.
Vikosi vya ulinzi na usalama vikiendelea kuwasaka wati waliohusika na shambulio dhidi ya kambi ya jesi ya Paramacay, nchini Venezuela. REUTERS/Marco Bello/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Upinzani, kwa upande wake, umeendelea kutoa shinikizo la kujiuzulu kwa rais Nicolas Maduro. Upinzani umewataka wafuasi wake kuzuia leo Jumanne barabara mbalimbali nchini kote kwa muda wa masaa sita.

Waziri wa Ulinzi akiwa pia Mkuu wa Majeshi,Jenerali Vladimir Padrino Lopez, amesema kuwa operesheni ya kijeshi inaendelea ili kumkamata afisa wa zamani wa kikosi cha Ulinzi wa Taifa, Juan Carlos Caguaripano na Luteni Jefferson Gabriel Garcia, wanaochukuliwa kuwa waandaaji wa shambulio la siku ya Jumapili dhidi ya kambi ya jeshi ya Paramacay, shambulio ambalo liliendeshwa na watu zaidi ya ishirini waliojihami kwa silaha za kivita.

Kwa mujibu wa Jenerali Padrino Lopez, ambaye alionekana katika video akizungukwa na magari matatu ya kijeshi, askari wenye silaha, watu hawa ni "maadui wa taifa".

Juan Carlos Caguaripano, alionekana kabla ya mashambulizi katika video iliyorushwa kwenye mitandao ya kijamii ambapo aliasema "kwa uasi halali" dhidi ya "udhalimu wa mauaji ya Nicolas Maduro" alifutwa kati katika jeshi mwaka 2014 kwa ajili kutotii amri ya rais huyo.

Alikataa kutambua vikwazo hivyo ambavyo alisema vikua vya "kisiasa". kisha kulaani "ukandamizaji" wa vikosi vya usalama wakati wa maandamano dhidi ya Maduro, ambapo wakati huo watu 43 waliuawa, naye Bw Caguaripano alikimbilia Panama.

Jefferson Gabriel Garcia ni askari aliekula njama na washambuliaji, ambaye alikua akihusika na kulinda ghala la silaha zilizoibiwa, kwa mujibu wa serikali ya Venezuela.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.