Pata taarifa kuu
VENEZUELA-KATIBA-HAKI

Ofisi ya Mashitaka yaomba kuvunjwa kwa Bunge la Katiba nchini Venezuela

Nchini Venezuela, Ofisi ya Mashitaka imeomba kuvunjwa kwa Bunge la Katiba ambalo linatazamiwa kuapishwa Ijumaa hii Agosti 4.

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro akihutubia wakati wa mkutano na wajumbe wa Bunge la Katiba tarehe 3 Agosti, 2017.
Rais wa Venezuela Nicolas Maduro akihutubia wakati wa mkutano na wajumbe wa Bunge la Katiba tarehe 3 Agosti, 2017. Palacio Miraflores
Matangazo ya kibiashara

Ombi hili linafuatia uamuzi wa Mwendesha Mashitaka Mkuu wa jamhuri, Luisa Ortega Díaz, ambaye aliomba kuanzishwa kwa uchugunz kuhusu uchunguzi wa Bunge la Katiba, ambapo upinzani ulitaja uchaguzi huo uligubikwa na wizi wa kura.

Wakurugenzi wanne wa Tume ya kitaifa ya Uchaguzi wanalengwa na uchunguzi huo. Wanatuhumiwa kula njama na rais Nicolas Maduro kuiba kura katika uchaguzi wa Jumapili na kutangaza kiwango kikubwa cha ushiriki ikilinganishwa na idadi halisi ya wapiga kura. Mwendesha mashtaka anachukulia madai ya kampuni ya Uingereza iliohusika nazoezi la kupiga kura.

Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Jamhuri, Luisa Ortega ambaye ni kinara wa maandamano dhidi ya Maduro, anataka uchunguzi kwa uchaguzi huo, pamoja na ushiriki wa wataalamu wa kimataifa. Kwa kusubiri hilo, Mwendesha Mashitaka Mkuu wa jamhuri ameomba raismi kuvunjwa kwa Bunge la Katiba ambalo linatazamiwa kuapishwa Ijumaa hii Agosti 4.

Wakati huo huo, rais Nicolas Maduro amesema akisisitiza kuwa Bunge la Katiba linapaswa kuapishwa Ijumaa hii kama alivyotangaza. Jitihada za Ofisi ya MAshitaka ina uwezekano mdogo wa kufanikiwa. Jitihada zake za awali zilifutwa na Mahakama Kuu, inayoshtumiwa na upinzani kuegemea utawala.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.