Pata taarifa kuu
VENEZUELA-USALAMA

Kura yafanyika katika hali ya vurugu Venezuela

Uchaguzi wa bunge la Katiba ulifanyika siku ya Jumapili nchini Venezuela, uchaguzi ambao uliitishwa na rais Nicolas Maduro. Baada ya kupiga kura, watu 537 watachaguliwa kwenye Bunge Maalum. Bunge hili litakua na mamlaka ya "kuandika katiba mpya."

Maandamano katika mji wa Caracas Jumapili Julai 30, 2017, wakati wa kura.
Maandamano katika mji wa Caracas Jumapili Julai 30, 2017, wakati wa kura. REUTERS/Carlos Garcia Rawlins
Matangazo ya kibiashara

Wapiga kura milioni 20 walitakiwa kushiriki uchaguzi huo ambao upinzani ulisusia. Zoezi hilo liligomewa na vyama vya upinzani vinavyompinga Rais Nicolas Maduro vyenye wabunge wengi katika bunge la Venezuela.. Upinzani unaona kwamba hiyo ni mbinu ya serikali ya kutaka kusalia madarakani."

Uchaguzi huu ulifanyika katika hali ya vurugu. Mgombea mmoja alipigwa risasi nyumbani kwake katika mji wa Ciudad Bolivar usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili na asubuhi, kiongozi wa upinzani aliuawa katika maandamano dhidi ya Bunge la Katiba katika mji wa Cumana. Katika mji mkuu wa Venezuela, Caracas, askari wasiopungua wanne walijeruhiwa katika mlipuko. Kwa jumla, watu wasiopungua kumi waliuawa katika siku inayotajwa kuwa ni umwagikaji damu baada ya miezi minne ya machafuko.

Matokeo ya awali yanatarajiwa kutangazwa licha ya maandamano makubwa yanayoendeshwa na upinzani.

Kumekuwa na mapambano kati ya polisi na waandamanaji ambao wanapinga Bunge hilo la Katiba ambapo wamekuwa wakiweka vizuizi barabarani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.