Pata taarifa kuu
VENEZUELA-USALAMA

Maduro atetea katiba mpya zikisalia siku tatu za uchaguzi

Nchini Venezuela, Kikao cha kufunga kampeni ya katiba mpya kilifanyika Ksiku ya Alhamisi Julai 27 katika mji mkuu wa nchi hiyo, Caracas. Rais Nicolas Maduro aliwataka wananchi wa Venezuela kuja kwa wingi kuunga mkono rasimu ya Bunge Maalum litakaloandika katiba mpya, ambapo uchaguzi umepangwa kufayika siku ya Jumapili Julai 30.

Hotuba ya Nicolas Maduro kumaliza kampeni za Bunge Maalum, Alhamisi, Julai 27, katika mji wa Caracas.
Hotuba ya Nicolas Maduro kumaliza kampeni za Bunge Maalum, Alhamisi, Julai 27, katika mji wa Caracas. REUTERS/Carlos Garcias Rawlins
Matangazo ya kibiashara

Upinzani umesem akuwa hautashiriki, kwa sababu unaona kuwa ni "wizi dhidi ya Katiba" na "mbinu ya serikali ya kubaki madarakani." Ni miezi 4 sasa tangu upinzani ukiandamana nchini kote ukipinga rasimu hiyo ya Katiba mpya, huku ukidai kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa haraka.

Kambi ya Maduro inasema kuwa "Bunge la Katiba litahakikisha hakikisha amani." Kwa siku hii ya mwisho ya kampeni, maelfu ya Wavenezuela walikusanyika kwenye mtaa wa Bolivar katikati ya mji mkuu kusikiliza hotuba ya Rais Maduro.

Kwenye mtaa wa Bolivar, Wavenezuela wengi walikua walivaa fulana zenye maandiko "njiani kuelekea Bunge la Katiba.

Wakati wa hotuba yake, Rais Maduro ametoa pendekezo kwa upinzani kuketi kwenye meza ya mazungumzo katika masaa yanayotangulia uchaguzi, kabla ya kuthibitisha kwamba uchaguzi utafanyika vizuri siku ya Jumapili Julai 30.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.