Pata taarifa kuu
VENEZUELA-MAREKANI-VIKWAZO

Maduro afutilia mbali vikwazo vya Marekani

Marekani imeweka vikwazo vya moja kwa moja dhidi ya "dikteta" Nicolas Maduro baada ya uchaguzi wa bunge la Katiba uliogubikwa na vifo kadhaa. Uchaguzi huu ulipendekezwa na rais Maduro mwenyewe, ambaye amepuuzia mbali "amri kutoka kwa Marekani."

Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro, apuuzia vikwazo vya Marekani dhidi yake.
Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro, apuuzia vikwazo vya Marekani dhidi yake. Miraflores Palace/REUTERS
Matangazo ya kibiashara

"Uchaguzi haramu wa siku ya Jumatatu unathibitisha kuwa Maduro ni dikteta ambaye anadharau matakwa yawananchi wa Venezuela," alisema Waziri wa Fedha wa Marekani Steven Mnuchin akinukuliwa siku ya Jumatatu usiku katika taarifa iliotolewa na wizara yake ambayo inatangaza "kuzuia mali zote" za rais wa Venezuela zinazopatikana nchini Marekani.

Ni nadra sana kwa serikali ya Marekani kuweka vikwazo dhidi ya rais wa nchi ya kigeni aliye madarani.

Bw Maduro ni rais wa nne kuwekewa vikwazo na Marekanibaada ya marais wa Syria Bashar al-Assad, Korea ya Kaskazini Kim Jong-Un na Robert Mugabe wa Zimbabwe.

Uamuzi wa Marekani ulichukuliwa siku moja baada ya uchaguzi wenye utata wa Bunge la Katiba uliopendekezwa narais wa Kisoshalisti, uchaguzi ambao uligubikwa na ghasia zilizosababisha vifo vya watu kumi.

"Mimi sitii amri kutoka kwa mabeberu, mimi sitii amri kutoka serikali za kigeni, mimi ni rais wa nchi huru," Bw Maduro alisema saa chache baadaye katika hotuba ya televisheni.

Kwa mujibu wa rais wa Venezuela, maamuzi ya serikali ya Marekani yanaonyesha "udhaifu wake, na chuki" baada ya uchaguzi wa Jumapili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.