Pata taarifa kuu
VENEZUELA-USALAMA

Shambulizi la kigaidi : Maduro alaumu upinzani

Rais wa Venezuela ametangaza kwamba watu zaidi ya ishirini walioendesha shambulio dhidi ya kambi ya jeshi kaskazini mwa nchi hiyo, walirejeshwa nyuma baada ya wawili miongoni mwao kuuawa na kumi kukamatwa. Wengine bado wanatafutwa, ameongeza rais Nicolas Maduro.

Rais wa Venezuela alitoa ufafanuzi kuhusu shambulizi dhidi ya kambi ya jeshi kaskazini mwa nchi, Agosti 06, 2017.
Rais wa Venezuela alitoa ufafanuzi kuhusu shambulizi dhidi ya kambi ya jeshi kaskazini mwa nchi, Agosti 06, 2017. Miraflores Palace/Handout via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Rais Maduro, ambaye alihutubia wananchi kwenye runinga ya taifa, shambulizi hilo lilisababisha vifo vya watu wawili waliuawa na mmoja kujeruhiwa. Watu wengine kumi, miongoni mwa walioendesha shambulio hilo, pia walikamatwa, ikiwa ni pamoja na raia tisa na afisa mmoja wa jshi, ambaye rais Madur amemtakja kuwa ni "mtoro"wa jeshi.

"Kwa sasa, kundi hilo limedhibitiwa," ameongeza rais Maduro. Nicolas Maduro anatambua kuwa waasi wamechukua sehemu kubwa ya silaha na risasi kutoka kambi ya jeshi na kwamba baadhi ya washambuliaji hawajapatikana.

Idadi kubwa ya askari wametumwa katika mji wa Valencia katika jaribio la kuwakamata washambuliaji hao. Kwa upande wa rais Nicolas Maduro, amesema shambulizi hilo ni la "kigaidiha", lililoandaliwa na upinzani na kusaidiwa kifedha na Marekani na Colombia.

Mgogoro waendelea

Viongozi wa upinzani, ikiwa ni pamoja Spika wa Bunge, Julio Borges, na mgombea urais wa zamani, Henrique Capriles, wanaendelea kukabiliana na rais Maduro. Viongozi hawa wamesema wamebadili mbinu mpya ya kupambana na rais Maduro.

Kwa upande wa upinzani, wamesema kutoridhika kwa vikosi vya kijeshi ni mfano tosha ambao unaonyesha jinsi gani nchi ya Venezuela inaendelea kupoteza. Upinzani unahofia kuongezeka kwa vitendo vingine katika siku zijazo dhidi Nicolas Maduro.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.