Pata taarifa kuu
VENEZUELA-MAANDAMANO-USALAMA

Maandamano ya upinzani kufanyika Jumatano hii Venezuela

Upinzani nchini Venezuela umewataka wafuasi wake kuingia mitaani Jumatano hii, April 19. Wapinzani wa Nicolas Madura wamewatolea wito wafuasi wao kwa maandamano katika mji wa Caracas lakini pia nchini kote. Lengo la maandamano hayo makubwa ni kutaka Uchaguzi Mkuu kufanyika mwaka huu.

Upinzani dhidi ya Rais wa Venezuela Nicolas Maduro wakiandamana mjini Caracas, Aprili 15, 2017.
Upinzani dhidi ya Rais wa Venezuela Nicolas Maduro wakiandamana mjini Caracas, Aprili 15, 2017. REUTERS/Carlos Garcia Rawlins
Matangazo ya kibiashara

April 19 tarehe inayokumbukwa sana nchini Venezuela kwa sababu ni tarehe vilipoanza vita vya kutetea uhuru wa Venezuela mwaka 1810. Lakini hasa mwaka huu upinzani unata kuongeza shinikizo kupitia maandamano baada ya Wiki takatifu iliyopita.

Tangu kutolewa kwa uamuzi wa Mahakama Kuu ambao ulizua hali ya sintofahamu nchini Venezuela ikiwa ni pamoja na ile kukubali mamlaka ya Bunge ambapo upinzani una idadi kubwa ya wajumbe, maandamano iyamendelea kuongezeka. Watu watano waliuawa wakati wa maandamano hayo na mamia walijeruhiwa na wengine kutiwa mbaroni.

"Maandamano ya Jumatano hii siya upinzani pekee, ni ya wananchi wote wa Venezuela, " Spika wa Bunge la Venezuela alisema siku ya Jumanneakibaini kwamba maandamano ya Jumatano hii yanafanywa dhidi ya Nicolas Maduro.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.