Pata taarifa kuu
UN-ANTONIO GUTERRES

Antonio Guterres Katibu Mkuu mtarajiwa wa UN

Waziri Mkuu wa zamani wa Ureno Antonio Guterres amehakikishiwa kuwa huenda akamrithi Ban Ki-moon kama Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, baada ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupiga kura isio rasmi Jumatano wiki hii. Bw Guterres huenda akachaguliwa kuanzia Alhamisi wiki hii.

Antonio Guterres.
Antonio Guterres. REUTERS/Denis Balibouse/File photo
Matangazo ya kibiashara

Balozi wa Urusi Vitaly Churkin, ambaye anaongoza Baraza la Usalama mwezi Oktoba, amewaambia waandishi wa habari baada ya kupiga kura kwamba Guterres anapewa nafasi kubwa ya kuchaguliwa kwenye nafasi hiyo.

Mwanadiplomasia huyu wa Urusi ametangaza kuwa uchaguzi rasmi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifala utafanyika Alhamisi hii ili kuthibitisha uchaguzi wa mgombea huyo, akiongeza kuwa anatarajia kuwa uteuzi utafanyika "hadharani".

"Tunamtakia mafanikio mema Bw Guterres katika utekelezaji wa majukumu yake ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika miaka hii mitano ijayo," amesema Churkin.

Wakati wa uchaguzi Jumatano wiki hii nchi tano wanachama wa kudumu, Uingereza, Marekani, Urusi, China na Ufaransa, ambao wana kura ya turufu, walipiga kura na kadi zenye rangi tofauti na ile ya wanachama wengine kumi. Katika uchaguzi uliopita wanachama wote, wa kudumu na wasio kuwa wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa walikua na kadi zinazofanana na zenye rangi moja.

Katika uchaguzi wa Jumatano Antonio Guterres aliungwa mkono na nchi 12 kwa jumla ya nchi 15, nchi mbili peke zilimpinga, na hivyo kupelekea uchaguzi wake kwenye nafasi ya Katibu Mkuu w Umoja wa Mataifa kukwama.

Hata hivyo mataifa matano yenye nguvu duniani hayakuzuia uchaguzi wa Bw Guterres, lakini nchi moja pekee ndio haikuonyesha msimamo wake.

Ban Ki-moon anamaliza muda wake wa mihula miwili ya miaka mitano kila muhula. Wagombea kwenye nafasi hiyo walikua kumi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.