Pata taarifa kuu
UN-UCHAGUZI-KAMPENI

Wagombembea 8 kwenye nafasi ya Katibu Mkuu wa UN

Wagombea 8 kwenye nafasi ya Katibu Mkuu wa Umoja wameamnza Jumanne hii kuonekana mbele ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa mahojiano ya ajira ya kipekee, kwa matumaini ya kumrithi Ban Ki-moon Januari, 2017.

Wagombea wanane wanaotaka kumrithi Ban Ki-moon kwenye nafasi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Wagombea wanane wanaotaka kumrithi Ban Ki-moon kwenye nafasi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. AFP / NICHOLAS ROBERTS
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mambo ya Nje wa Montenegro Igor Luksic, mwenye umri wa miaka 39, ambaye ni mdogo kabisa kwa jumla ya wagombea kwenye nafasi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ndio alianza kupokelewa na Mkutano Mkuu wa Umoja wa mataifa, akijionyesha kama mwakilishi wa "nchi ndogo lakini fahari katika historia ulimwenguni."

Akionekana kama mwenye hasira, Igor Luksic amezungumza kwa Kingereza na Kifaransa kwa masuala waliokubaliana kuhusu changamoto za sasa (ugaidi, wakimbizi, upokonyaji wa silaha, haki za binadamu, nk ...), kabla ya kuwashukuru wanadiplomasia walioshiriki kikao hicho katika lugha zote za kazi za Umoja wa Mataifa.

Ufaransa inasisitiza kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa awe anazungumza zaidi au kiasi lugha ya nyumbani (Kifaransa).

Awali, Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mogens Lykketoft, alikumbusha kuwa ni zoezi la kwanza la aina yake katika historia ya Umoja wa Mataifa.

Alimtaka kama vipaumbele mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi, uendelezaji wa amani, pamoja na "kuweka shinikizo juu mataifa yenye nguvu," au "mageuzi" ya Umoja wa Mataifa.

Ban Ki-moon anaondoka mamlakani mwishoni mwa mwaka huu baada ya kuhudumu mihula miwili ya miaka mitano.

Kwa sasa wanaume wanne na wanawake wanne wanawania kwenye nafasi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Miongoni mwa wagombea wanopewa nafasi kubwa ya kushikilia wadhifa huo ni pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Mbulgaria Irina Bokova, aliyekuwa Waziri Mkuu wa New Zealand Helen Clark, ambaye anaongoza Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa, na aliyekuwa Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi, Mreno, Antonio Guterres.

Wengine wanaosalia ni pamoja na Rais wa zamani wa Slovenia Danilo Türk na Mawaziri wanne wa Mambo ya Nje wa zamani au wa sasa kutoka nchi za Balkan - Vesna Pusic (Croatia), Natalia Gherman (Moldova), Srgjan Kerim (Makedonia) na Igor Luksic (Montenegro).

Wagombea hao wataendelea kusikilizwa kwa muda wa siku tatu mfululizo. Kila mgombea atakuwa na masaa mawili ya kuweka wazi sera zake na kujibu maswali, kwanza ya wanadiplomasia na kisha asasi za kiraia, kwa video. Maelfu ya maswali yamependekezwa kutoka nchi 70, lakini yalipunguzwa na kusalia thelathini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.