Pata taarifa kuu
UN-BAN KI MOON

Ban Ki Moon aunga mkono uteuzi wa mwanamke kurithi nafasi yake

Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, amesema anatamani kuona mwanamke akipewa nafasi ya kuongoza taasisi hiyo nyeti duniani, wakati yeye atakapomaliza muda wake.

Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon ambaye anapendekeza nafasi yake irithiwe na mwanamke.
Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon ambaye anapendekeza nafasi yake irithiwe na mwanamke. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Ban Ki Moon amesema "huu ni muda muafaka" kwa mwanamke kuongoza taasisi hii, baada ya miaka 70 ya umoja wa Mataifa iliyotawaliwa na watawala ambao ni wanaume.

Kati ya wagombea 11 ambao wamejitokeza kuwania kiti hicho kwenye uchaguzi wa mwaka huu, wagombea watano ni wanawake.

Katibu mkuu ni lazima apendekezwe na nchi 15 wanachama wa baraza la usalama na kisha kuchaguliwa na nchi 193 wanachama wa umoja wa Mataifa.

Katibu mkuu mpya wa umoja wa Mataifa anatarajiwa kutangazwa wakati wa kipindi cha majira ya Kipupwe, lakini kikawaida katibu mkuu mpya ubadilishwa kutokana na ukanda.

Ulaya mashariki na Urusi ndio maeneo pekee ambayol hayajawahi kutoa katibu mkuu wa umoja wa Mataifa, ambapo wajumbe wake wanataka safari hii katibu mkuu atoke kwenye eneo lake.

Katibu mkuu Ban Ki Moon hakumtaja wazi ni mgombea gani ambaye anamuunga mkono, lakini akasisitiza kuwa atamuunga mkono mwanamke ambaye atalaeta mabadiliko kwenye umoja huo.

Katika kura za maoni zilizofanyika hivi karibuni, Antonio Guterres waziri mkuu wa zamani wa Ureno na pia mkuu wa shirika la wakimbizi duniani UNHCR, anapewa nafasi kushinda kiti hicho.

Wanawake wanaopewa nafasi kushika nafasi hiyo ni pamoja na Irina Bokova wa Bulgaria na Susan Malcorra wa Argentina ambao wamefikia nafasi ya tatu katika orodha ya viwango.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.