Pata taarifa kuu
DUNIA-WFP-CORONA-AFYA-CHAKULA

Umoja wa Mataifa: Ulimwengu wakabiliwa na kitisho cha janga la kibinadamu

Umoja wa Mataifa umeonya kuwa kutokana na mgogoro unaosababishwa na ugonjwa hatari wa Covid-19, ulimwengu unakabiliwa na tishio la janga la kibinadamu.

Maafisa wa afya wakipulizia dawa kudhibiti kuenea kwa virusi vya katika soko kuu la jiji la Nairobi, Kenya Aprili 19, 2020.
Maafisa wa afya wakipulizia dawa kudhibiti kuenea kwa virusi vya katika soko kuu la jiji la Nairobi, Kenya Aprili 19, 2020. REUTERS/Njeri Mwangi
Matangazo ya kibiashara

Wakati ugonjwa huo umeua zaidi ya watu 174,000 ulimwenguni tangu kuzuka nchini China mwezi wa Desemba 2019, kulingana na ripoti iliyotolewa Jumanne Aprili 21 na shirika la habari la AFP, wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limeonya kuhusu athari ya ugonjwa huo katika suala la chakula.

"Idadi ya watu wanaokabiliwa na uhaba wa chakula inaweza kuongezeka mara mbili kwa sababu ya janga la Covid-19, na kufikia zaidi ya milioni 250 ifikapo mwishoni mwa mwaka 2020," WFP imeonya.

Ripoti ya kila mwaka ya Kimataifa kuhusu Migogoro ya Chakula imesema kuwa uhaba wa chakula tayari ulikuwa mkubwa mwaka jana kabla ya mlipuko wa ugonjwa hatari wa Covid-19.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.