Pata taarifa kuu
SAUDI ARABIA-CORONA-AFYA

Misikiti miwili mikuu ya Saudi Arabia kufungwa wakati wa mfungo wa Ramadhan

Mamlaka nchini Saudi Arabia imetangaza kwamba Misikiti miwili mikuu itaendelea kufungwa wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan ambao unaanza wiki hii.

Saudi Arabia ndiko inakopatikana misikiti miwili mitakatifu zaidi: Masjid al-Haram, mjini Makka, ambao ndiyo kituo cha Ibada ya kila mwaka ya Hajj, na Masjid an-Nabawi – au Msikiti wa Mtume, katika mji wa Madina.
Saudi Arabia ndiko inakopatikana misikiti miwili mitakatifu zaidi: Masjid al-Haram, mjini Makka, ambao ndiyo kituo cha Ibada ya kila mwaka ya Hajj, na Masjid an-Nabawi – au Msikiti wa Mtume, katika mji wa Madina. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Swala zitafanyiika katika misikiti hiyo miwili lakini waumini hawataruhusiwa kushiriki ibada hizo katika kuzuia kusambaa kwa virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19, uongozi misikiti huyo aumesema.

Saudi Arabia ni nchi ya jangwa inayojumuisha sehemu kubwa ya rasi ya Arabuni, pamoja na pwani za Bahari ya Sham na Ghuba ya Uajemi.

Ikifahamika kuwa ndiyo mahala ulipozaliwa Uislamu, Saudi Arabia ndiko inakopatikana misikiti miwili mitakatifu zaidi: Masjid al-Haram, mjini Makka, ambao ndiyo kituo cha Ibada ya kila mwaka ya Hajj, na Masjid an-Nabawi – au Msikiti wa Mtume, katika mji wa Madina, alikozikwa Mtume Muhammad (S.A.W).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.