Pata taarifa kuu

Wataalamu wakiri kuwa ugonjwa wa Kansa waathiri watu wengi duniani

Kansa au kwa jina jingine, Saratani, ni kundi la magonjwa yanayosababishwa na mgawanyiko usio sawa na usiodhibitika wa seli na kuunda uvimbe unaovamia na kuzidhuru tishu za mwilini. Kansa isiyotibiwa, inaweza kuwa ugonjwa unaoshambulia tishu nyingine mwilini na kusababisha kifo.

Jinsi chembechembe za saratani zinavyokuwa mwilini.
Jinsi chembechembe za saratani zinavyokuwa mwilini. © iStockphoto
Matangazo ya kibiashara

Saratani ni neno la Kirabu (سرطان) au kansa kwa Kingereza (cancer) ni aina za ugonjwa unaoanzishwa na seli za mwili zinazoanza kujigawa yaani kukua bila utaratibu na bila mwisho.

Ukuaji huu unaleta uvimbe mwilini unaozidi kuwa mkubwa hadi inabana viungo vya mwili kama neva, mishipa ya damu, ubongo, mapafu, maini, utumbo na kadhalika na kuzuia visifanye kazi.

Asili ya neno kansa linatokana na daktari bingwa wa Ugiriki aliyeishi kati ya miaka 460 na 370 (K.K) anayejulikana kwa jina la Hippocrates. Hippocrates alitumia maneno 'Carcinos' na 'Carcinoma' kuelezea uvimbe unaotengeneza mchubuko (Carcinos) kwa upande mmoja, na uvimbe usiotengeneza mchubuko (Carcinoma) kwa upande wa pili.

Pamoja na hayo kansa / saratani huwa na tabia za kujisambaza mwilini mahali pengi baada ya muda fulani na kusababisha kutokea kwa vimbe nyingi mwilini vinavyoendelea kukua hovyo. Kama uvimbe hauna uwezo wa kusambaa seli zake mwilini na kusababisha vimbe mpya si saratani.

Ajali ni kitu kinachotokea bila kukusudiwa na kupangwa kwa wakati fulani. Saratani ni mojawapo ya ajali zinazoweza kutokea bila kudhaniwa. Mfano ni saratani ya damu ambayo husababishwa na vitu kama moto mkali wa kemikali au kunusa kemikali huweza kusababisha saratani ya pua au koo.

Kansa inaweza kutokea kwa mtu yeyote lakini hutokea zaidi kwa watu wenye umri mkubwa na watu wanaoathiriwa na kemikali mbalimbali. Katika nchi zilizoendelea ambako wanachi hufikia umri mkubwa saratani iko kati ya sababu kuu za kifo.

Uchunguzi na matibabu ya kansa ni utaalamu wa onkolojia ndani ya somo la tiba.

Udhibiti wa saratani unamaanisha kutibu ugonjwa wa saratani au kansa

Kwa mujibu wa Dkt Sophonie Niyondavyi, anayeendesha shughuli zake mjini Bujumbura, nchini Burundi, Saratani inaweza kutibiwa kwa kufanyia upasuaji, tibakemo, matibabu kwa njia ya eksirei, matibabu ya tibamaradhi, matibabu ya monokloni ya kingamwili au njia zingine. Uchaguzi ya matibabu hutegemea mahali uvimbe ulipo na daraja lake na hatua ya ugonjwa huo, pamoja na hali ya jumla ya mgonjwa (hali ya utendaji). Idadi kadhaa ya matibabu ya saratani ya majaribio hayajatengenezwa kikamilifu.

Kuondolewa kikamilifu kwa saratani // kansa bila kuharibu sehemu zingine za mwili ndilo lengo la matibabu. Wakati mwingine jambo hili linaweza kutimizwa kwa upasuaji, lakini hulka wa saratani ya kuvamia tishu zilizo karibu au kuenea kwenye maeneo ya mbali kupitia uenezi mdogo sana kiasi kwamba hauwezi kuonekana kwa macho mara nyingi huzuia ufaafu wake. Ufaafu wa tibakemo mara nyingi huzuiwa na kiwango cha kusumisha tishu zingine katika mwili. Mnururisho unaweza pia kuharibu tishu ya kawaida.

Kwa sababu neno "saratani // kansa" linarejelea jamii ya magonjwa, hakuna uwezekano kwamba daima kutawahi kuwa na aina moja ya "tiba ya kansa // saratani" zaidi ya vile kutawahi kuwa na tiba moja ya magonjwa yote ya kuambukiza. Vizuizi vya Anjiojenesisi viliwahi kufikiriwa kuwa na uwezo wa kuwa kama matibabu ya "risasi fedha (silver bullet)" yanayoweza kutumiwa katika aina nyingi za saratani, lakini jambo hili halijadhihirika katika utendaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.