Pata taarifa kuu
MAREKANI-MEXICO-SAYANSI

Kwa mara ya kwanza, mtoto azaliwa kutoka mbegu za watu watatu

Jarida la kisayansi la American Society ya Uzazi Medicine lilitangaza Jumanne Septemba 27 kuzaliwa mwezi Aprili kwa mtoto aliyeetengenezwa kwa kutumia mbinu ya uzazi wa mbegu za watu watatu tofauti.

Mwamko mpya wa kimatibabu kuwezesha kuzaliwa kwa mtoto kutoka mbegu za watu watatu tofauti  mwezi Aprili 2016.
Mwamko mpya wa kimatibabu kuwezesha kuzaliwa kwa mtoto kutoka mbegu za watu watatu tofauti mwezi Aprili 2016. abdelmassih.com.br/Wikipédia
Matangazo ya kibiashara

Madaktari wa Marekani walichukua hatua hiyo kuhakikisha kuwa mtoto huyo wa kiume atakuwa huru kutokana na hali ya jeni ambayo mamake kutoka Jordan anabeba katika jeni zake.

Mtoto huyo wa kiume mwenye umri wa miezi mitano sasa ana chembe chembe za DNA kutoka kwa mamake, babake pamoja na jeni za mfadhili.

Mitochondria ni vyumba vidogo vidogo ndani ya kila seli ambavyo hubadili chakula kuwa nguvu inayotumika mwilini.

Wataalam wanasema kuwa hatua hiyo ni mwamko mpya wa kimatibabu na inaweza kusaidia familia nyingine zilizo na hali za jeni zisizokuwa za kawaida.

Lakini wameonya kuwa uchunguzi wa mara kwa mara wa mbinu hiyo mpya ya kiteknolojia inayoitwa ufadhili wa Mitochondrial unahitajika.

Wanasayansi waliohusika katika shughuli hiyo walisafiri hadi Mexico kwa sababu huko hakuna sheria za kuzuia shughuli kama hiyo ya kimatibabu.

Walichukua sehemu muhimu za chembe za kinasaba (DNA) kutoka kwa yai la mama, na DNA ya mitochondria kutoka kwa yai la mfadhili na kuunda yai lenye afya ambalo lilitungishwa mbegu kutoka kwa baba.

Matokeo yake ni kuzaliwa kwa mtoto mwenye 0.1% ya DNA kutoka kwa mfadhili na jeni nyingine zote, zinazoamua sifa kama vile rangi ya nywele na macho kutoka kwa mama na baba.

Dkt John Zhang, mkurugenzi wa kimatibabu katika hospitali ya New Hope Fertility Centre jijini New York City, anasema yeye na wenzake walitumia njia hiyo kupata viinitete vitano, lakini wakastawisha kimoja tu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.