Pata taarifa kuu
UN-AFYA

UN: hatua kali za usafi kwa askari wa kulinda amani

Umoja wa Mataifa (UN) umesema kuwa hatua zimezochukuliwa ili kupanga vipimo vya afya kwa ajili ya askari wa kulinda amani kabla ya kutumwa katika nchi zinazokabiliwa na migogoro.

Wagonjwa wa Kipindupindu wakipanga foleni katika hospitali ya Saint-Marc kaskazini mwa mji wa Port-au-Prince, Oktoba 24, 2010.
Wagonjwa wa Kipindupindu wakipanga foleni katika hospitali ya Saint-Marc kaskazini mwa mji wa Port-au-Prince, Oktoba 24, 2010. AFP / Thony Belizaire
Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Mataifa unataka kuhakikisha kuwa askari wake wote wanapewa chanjo dhidi ya kipindupindu na homa ya manjano.

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Atul Khare amesema wakati wa ziara yake nchini Nepal kwamba hatua hizo zitachukuliwa kwa raia na askari wa kulinda amani.

Mapema mwezi huu, Umoja wa Mataifa, hatimaye ulikiri kwamba ulichangia katika kuenea kwa ugonjwa wa kipindupindu nchini Haiti.

Ugonjwa huo umeua watu 10 000 katika kipindi cha miaka sita.

Tafiti za kisayansi zimeonyesha kuwa askari wa Umoja wa Mataifa kutoka Nepal ndio chanzo cha ugonjwa huo ambao ulienea kutoka katika kambi ya Umoja wa Mataifa kwa njia ya mabomba ya maji taka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.