Pata taarifa kuu

Jeshi la Niger lashambulia kwa mabomu 'magaidi' baada ya kupoteza wanajeshi sita

Wanajeshi sita wa Niger waliuawa kwa bomu katika eneo la Inates, karibu na Mali, jeshi la Niger limetangaza siku ya Alhamisi, ambalo liliongeza kuwa "limewatenga" angalau "magaidi" kumi katika mashambulizi ya anga katika pande zote za mpaka.

Niger pia inakabiliwa, katika sehemu yake ya kusini-mashariki karibu na Nigeria, na makundi ya wanajihadi wenye silaha ya Boko Haram na Islamic State katika Afrika Magharibi (ISWAP).
Niger pia inakabiliwa, katika sehemu yake ya kusini-mashariki karibu na Nigeria, na makundi ya wanajihadi wenye silaha ya Boko Haram na Islamic State katika Afrika Magharibi (ISWAP). AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi hao sita walikufa "mwanzoni mwa juma" wakati gari lao la doria "lililokuwa linarudi kutoka Inates" liliporuka kwenye baada ya kukanyaga bomu la kutegwa ardhini karibu na kijiji cha Tingara (kusini-magharibi), inabainisha Wizara ya Ulinzi ya Niger katika taarifa yake ya hivi punde. Askari wengine walijeruhiwa na kuhamishwa kwa helikopta hadi Niamey, wizara imeogeza katika taarifa.

Ufuatiliaji wa angani ulifanya iwezekane "kuwapata magaidi watatu waliohusika" katika "kitendo hiki cha kikatili", inaongeza wizara hiyo. "Walifuatwa hadi kwenye kitongoji" ambapo walijiunga "karibu na washirika wengine ishirini" na "shambulio la anga" lilifanyika, ambalo "liliwaangamiza" (liliwaua) kadhaa kati yao na kuharibu vifaa vya kijeshi, imebainisha Wizara ya Ulinzi ya Niger.

Katika mchakato huo, shambulio lingine la anga lililenga "kundi la magaidi" katika eneo la Mali la Amalaoulaou, ambalo lilifanya iwezekane "kuwatia nguvuni wapiganaji wanane" na "kuharibu vifaa vya vya kijeshi", inaendelea taarifa ya wizara.

Inates iko katika eneo la Tillabéri, ambalo limekuwa maficho ya wanajihadi wa Sahel, wakiwemo wale wa Islamic State katika Sahara Kubwa (EIGS) na Al-Qaeda. Mnamo mwezi wa Desemba 2020 huko Inates, wanajeshi 71 wa Niger waliuawa katika shambulio kwenye kambi yao, lililodaiwa na EIGS.

Tangu mwisho wa mwezi wa Julai 2023, Niger imekuwa ikiongozwa na wanajeshi waliochukua madaraka kwa nguvu kwa lengo lililowekwa la kukomesha ghasia za wanajihadi. Lakini mashambulizi yanaendelea. Mwishoni mwa mwezi wa Machi, shambulio la wanajihadi dhidi ya jeshi la Niger liligharimu maisha ya wanajeshi 23 karibu na Bankilaré, katika eneo lililo karibu na Burkina Faso na Mali, lililovamiwa na makundi ya kijihadi ambayo yanazidisha mashambulizi katika eneo hilo.

Niger pia inakabiliwa, katika sehemu yake ya kusini-mashariki karibu na Nigeria, na makundi ya wanajihadi wenye silaha ya Boko Haram na Islamic State katika Afrika Magharibi (ISWAP).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.