Pata taarifa kuu

Ituri: Watu 34 waliuawa na wanamgambo wa CODECO katika muda wa siku 3 huko Djugu

Katika muda wa siku tatu, wanamgambo wa CODECO waliwaua watu wasiopungua thelathini na watatu katika eneo la Djugu, viongozi wa jamii katika eneo hilo walisema Jumatatu Aprili 8.

Juni 2023. Kuna msongamano katika kambi ya Rhoe, katika eneo la Djugu (jimbo la Ituri, nchini DRC) ambapo makumi ya maelfu ya watu waliokimbia makazi yao wanateseka kwa njaa.
Juni 2023. Kuna msongamano katika kambi ya Rhoe, katika eneo la Djugu (jimbo la Ituri, nchini DRC) ambapo makumi ya maelfu ya watu waliokimbia makazi yao wanateseka kwa njaa. © Coralie Pierret/RFI
Matangazo ya kibiashara

Raia 15, wakiwemo wanawake watatu na mtoto mchanga wa siku kumi na nne, walichomwa wakiwa hai Jumatatu Aprili 8 na kundi la wanamgambo katika kijiji cha Andissa, takriban kilomita 40 kutoka wilaya ya Mongbwalu.

Kulingana na viongozi wa jamii ya eneo hilo, watu hawa walichukuliwa mateka na wanamgambo siku ya Jumamosi Aprili 6 ili kusafirisha bidhaa zilizoporwa.

Kati ya mateka hawa, watatu waliachiliwa. Lakini wawajapatikana.

Kulinana na Radio OKAPI, vyanzo hivyo vinaripoti kwamba wanamgambo wa CODECO kutoka kundi la "Hekalu Jema la Mungu", wakitoka katika vijiji vya Andisa, Buraki, Wazabo na Dragi, walishambulia siku ya Jumamosi Aprili 6 kijiji cha Galayi kwenye kingo za Mto Ituri katika eneo la Banyali Kilo.

Walifyatua risasi kadhaa na kuwaua watu kumi na wanane, wakiwemo wanawake watano.

Miili ya wahanga hao ilipatikana siku ya Jumatatu, ikielea kwenye mto Ituri.

Mwanajeshi, aliyejeruhiwa wakati wa shambulio hili, alifariki siku hiyo ya Jumamosi katika hospitali ya Mongbwalu.

Kifo chake kinafikisha thelathini na nne idadi ya watu waliouawa na wanamgambo hawa katika eneo hili tangu Jumamosi Aprili 6.

Mkuu wa sekta ya Banyali Kilo anaiomba Serikali kuimarisha idadi ya wanajeshi, ili kurejesha mamlaka ya Serikali katika eneo hili.

Pia anatoa wito wa kuanzishwa kwa operesheni za kuwasaka wanamgambo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.