Pata taarifa kuu

Wanajeshi watatu wa Tanzania wauawa kwa bomu nchini DRC

Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) imetangaza siku ya Jumatatu vifo vya wanajeshi wake wanne waliotumwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wakiwemo Watanzania watatu waliouawa kwa bomu siku ya Alhamisi wiki iliyopita kwa mujibu wa chanzo kutoka Kongo.

Hii si mara ya kwanza kwa askari wa kulinda amani wa Tanzania kuuawa katika kutekeleza majukumu yao nchini DRC.
Hii si mara ya kwanza kwa askari wa kulinda amani wa Tanzania kuuawa katika kutekeleza majukumu yao nchini DRC. REUTERS/Emmanuel Herman
Matangazo ya kibiashara

Wa nne, raia wa Afrika Kusini, alifariki hospitalini kufuatia matatizo ya kiafya, SADC imesema katika taarifa yake, na kuongeza kuwa wanajeshi wengine watatu wa Tanzania walijeruhiwa.

Tangu mwezi Desemba, SADC imepeleka kikosi katika mkoa wa Kivu Kaskazini kinachoundwa na wanajeshi kutoka Afrika Kusini, Tanzania na Malawi, kusaidia vikosi vya serikali ya DRC kupambana na waasi wa M23 ambao, kwa msaada wa Rwanda, wameteka sehemu kubwa za mkoa huo. SADC ilitangaza hasara yake ya kwanza mnamo Februari 15, wakati wanajeshi wawili wa Afrika Kusini waliuawa kwa bomu karibu na Goma, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini.

Ujumbe wa SADC nchini DRC (SAMIDRC) "unasikitika kujulisha umma" kwamba askari wake watatu kutoka Tanzania waliuawa na wengine watatu kujeruhiwa "wakati bomu lilipoanguka karibu na kambi walimokuwa," SADC imesema siku ya Jumatatu. SAMIDRC pia inatangaza "kwamba mwanajeshi wa Afrika Kusini alikufa alipokuwa akitibiwa katika hospitali ya Goma kwa matatizo ya afya", inaongeza taarifa kwa vyombo vya habari. Kwa sharti la kutotajwa jina, chanzo cha usalama cha Kongo kimeeleza kuwa wanajeshi hao wa Tanzania waliuawa na kujeruhiwa katika kambi ya Mubambiro, iliyoko takriban kilomita ishirini magharibi mwa Goma huko Sake, jiji linalochukuliwa kuwa la kimkakati katika barabara ya kuelekea mji mkuu wa mkoa.

Kulingana na chanzo kingine, karibu na mkoa wa Kivu Kaskazini, mauaji haya yalifanyika mnamo Aprili 4. Wanajeshi wawili wa Afrika Kusini waliuawa katika sehemu moja mwezi Februari. Chanzo cha habari katika mkoa huo, ambacho pia hakikutaka kutajwa jina, kimeongeza kuwa hafla ya kutoa heshimaza mwisho kwa wanajeshi hao, ambayo alishiriki, ilifanyika Jumatatu katika makao makuu ya SAMIDRC, Goma.

Katika ujumbe uliotumwa mwishoni mwa wiki kwa wafanyakazi wake, ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC (MONUSCO) ulielezea hali ya usalama "inayozidi kuwa tete" mashariki mwa DRC. M23 "imefika kwenye viunga vya kaskazini mwa Sake", ulisema ujumbe wa Umoja wa Mataifa, na kuongeza kuwa "watu wengine wenye silaha wameonekana katika mbuga ya wanyama ya Virunga na wanatishia kukata barabara ya Goma-Sake".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.