Pata taarifa kuu

RDC: Mapigano mapya yameripotiwa katika maeneo ya Bwito Rutshuru

Nairobi – Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kuanzia mapema leo asubuhi mapigano mapya yameripotiwa kati ya jeshi la serikali na waasi wa M 23 katika maeneo ya Bwito, Wilayani Rutshuru, jimboni Kivu Kaskazini.

Mapigano haya yamesababisha mamia ya watu kuyakimbia makaazi yao, na kuelekea maeneo ya Kanyabayonga wakipitia Kibirizi
Mapigano haya yamesababisha mamia ya watu kuyakimbia makaazi yao, na kuelekea maeneo ya Kanyabayonga wakipitia Kibirizi © RFI/Paulina Zidi
Matangazo ya kibiashara

Raia wa kawaida wanasema waliamkia mapigano makali katika vijiji vinavyozunguka mji wa Nyanzale na eneo la Mabenga, hali ambayo inaendelea kuzua wasiwasi.

Ripoti zinasema kuanzia saa 11 Alfajiri, milio ya risasi na sauti ya vilipuzi vilisikika katika kijiji cha Matete, kilichopo kati ya Kishishe na Kirima, lakini pia katika vijiji vingine vya Kisoko, Mubirubiru na Lwahanga, vinavyozingira mji wa Nyanzale.

Baadaye, mabomu mawili yalirushwa kwenye kijiji cha Kihondo, karibu na kambi ya jeshi la kulinda amani la Umoja wa Mataifa na kusababisha majeraha ya watu kadhaa.

Mapigano haya yamesababisha mamia ya watu kuyakimbia makaazi yao, na kuelekea maeneo ya Kanyabayonga wakipitia Kibirizi.

Viongozi wa mashirika ya kiraia, wanasema kufuatia siku kadhaa za utulivu, mapigano hayo mapaya yamejiri baada ya waasi wa M 23 kujipanga rena na kuanza kuwashambulia wanajeshi wa FARDC.

Haya yanajiri baada ya viongozi wa majeshi kutoka nchi za Afrika Kusini, Tanzania, Malawi na Burundi, nchi ambazo zinaunda kikosi cha pamoja cha kulinda amani kilichoko chini ya Jumuiya ya SADC, SamiDRC, mwishoni mwa juma lililopita, kukamilisha ziara yao mashariki mwa nchi hiyo na kutoa hakikisho la kurejesha usalama kwa kushirikiana na vikosi vya Serikali, FARDC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.