Pata taarifa kuu

Zambia: Njaa inaathiri zaidi ya watoto milioni moja, yaaonya shirika lisilo la kiserikali

Zambia imekuwa ikikosa mvua kwa zaidi ya miezi miwili. Athari za mfumo wa hali ya hewa ya El Niño, iliyozidishwa na mabadiliko ya tabianchi. Ukame umeharibu nusu ya mazao.

Shirika la mpango wa chakula WFP, linasabaza msaada wa chakula huko Simumbwe, Zambia (picha ya kielelezo).
Shirika la mpango wa chakula WFP, linasabaza msaada wa chakula huko Simumbwe, Zambia (picha ya kielelezo). AFP - GUILLEM SARTORIO
Matangazo ya kibiashara

Leo, nchini Zambia, zaidi ya watoto milioni moja wana njaa, linaonya shirika lisilo la kiserikali la Save The Children, ambalo limekusanya ushuhuda hasa magharibi mwa nchi hiyo. Kulingana na Malama Mwila, meneja wa sera na utetezi wa kikanda wa shirika hili lisilo la kiserikali, Mashariki na Kusini mwa Afrika, ambaye anajibu maswali kutoka kwa Lucile Gimberg, "hii ina maana kwamba kila siku, wanakula mlo mmoja tu kwa siku. Na tena, chakula hiki hakiwezi kuitwa chakula! »

"Bila chakula, wanalala"

"Baadhi ya watu," Malama Mwila anaongeza, "hutumia saa nyingi kwenye savanna au msituni kutafuta matunda ya mwituni kula. Vinginevyo, wanakula tunachokiita hapa mashwa. Ni aina ya mizizi ya majini ambayo huchemshwa ili iweze kuliwa. "

“Tunachokiona katika jamii zilizoathirika ni kwamba watoto hawawezi kwenda shule wakiwa na tumboni hama kitu. Hawawezi kuzingatia. Mama mmoja alituambia kwamba anapowatazama watoto wake, anafikiri kwamba ni wagonjwa. Lakini kwa kweli wanahitaji kula tu. Bila chakula, wanalala, ni utaratibu wa asili unapokuwa na njaa,” anahitimisha meneja huyu wa kikanda wa sera na utetezi wa shirika lisilo la kiserikali la Save The Children.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.