Pata taarifa kuu
UWEKEZAJI-UCHUMI

Zambia yafikia makubaliano ya 'kihistoria' na wakopeshaji binafsi

Zambia imefikia makubaliano ya "kihistoria" na wakopeshaji wake binafsi wanaoshikilia dola bilioni 3.5 katika Eurobond, na kuondoa kikwazo kikubwa katika mazungumzo ya kurekebisha deni lake kubwa, Rais Hakainde Hichilema ametangaza siku ya Jumatatu.

Upinde wa mvua juu ya Maporomoko ya Victoria kwenye Mto Zambezi kwenye mpaka wa Zambia na Zimbabwe mnamo Juni 29, 2018.
Upinde wa mvua juu ya Maporomoko ya Victoria kwenye Mto Zambezi kwenye mpaka wa Zambia na Zimbabwe mnamo Juni 29, 2018. © AFP
Matangazo ya kibiashara

"Ukurasa wa historia umeandikwa! Tuna furaha kutangaza makubaliano na wamiliki wetu wa Eurobond," Bw. Hichilema ametangaza kwa ushindi juu ya marekebisho ya "zaidi ya dola bilioni 3.5" za deni.

"Hatua muhimu ambayo sote tulikuwa tukiingoja kwa kukosa subira. Urekebishaji mpya wa Eurobond umeafikiwa," Waziri wa Fedha Situmbeko Musokotwane pia amethibitisha kwenye X.

Zambia ilikuwa nchi ya kwanza barani Afrika kutolipa deni lake la umma mnamo mwaka 2020 baada ya kuzuka kwa janga la UVIKO-19. Lusaka ilifikia makubaliano kimsingi na wakopeshaji wake wa umma mwezi Juni kuhusu urekebishaji wa dola bilioni 6.3 katika deni la nje.

Bill Gates na Jeff Bezos wanapanga kuwekeza katika mgodi nchini Zambia

Mwezi Desemba, Bw. Hichilema alisema kwamba karibu asilimia 98 ya wadai rasmi wametia saini mkataba wa makubaliano ya kurekebisha deni la nchi hiyo ya kusini mwa Afrika linalokadiriwa kufikia dola bilioni 32.8 mwishoni mwa 2022, zikiwemo dola bilioni 18.6 kutoka kwa wakopeshaji wa kigeni kama China, mkopeshaji wake mkuu.

Hadi sasa, majadiliano na "wadai binafsi ambao wanawakilishwa na wenye dhamana" bado yamekwama, Bw. Hichilema alilalamika, akiwashutumu kuchelewesha mchakato huo.

Kulingana na mojawapo ya vifungu vya mkataba huo uliohitimishwa katika mfumo wa kurekebisha deni kwa nchi maskini zaidi uliokubaliwa na kundi la G20, haungeweza kutumika ikiwa sekta ya kibinafsi haikufanya juhudi kulinganishwa katika makubaliano yoyote ya marekebisho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.