Pata taarifa kuu

Rais Hichilema wa Zambia amekutana na mwenzake wa China Xi jijini Beijing

Rais wa Zambia Hakainde Hichilema amekutana na mwenzake wa China Xi Jinping, ambapo viongozi hao wamejadiliana kuhusu ushirikiano wa kiuchumi. 

China ni mkopeshaji mkubwa wa Zambia
China ni mkopeshaji mkubwa wa Zambia © Hakainde Hichilema
Matangazo ya kibiashara

Kikao hiki kinakuja wakati huu Zambia inayosumbuliwa na madeni ya kimataifa, ikitafuta namna ya kuangalia upya na inavyoweza kuyalipa. 

Kwa ujumla Zambia inadaiwa na mataifa ya kigeni, na mashirika ya Kimataifa Dola Bilioni 32.8 kufikia mwisho wa mwaka uliopita, na ilishindwa kulipa deni linalokadiriwa kuwa Dola Bilioni 18.6 wakati wa kipindi cha Uviko 19 mwaka 2020. 

Rais China, Xi amesema urafiki wa nchi yake na Zambia unasalia imara licha ya changamoto inazokumbana nazo kiuchumi. 

China imewekeza kwa kiasi kikubwa kwenye sekta ya madini nchini Zambia na kutoa mkopo wa kujenga  miundombinu kama barabara, viwanja vya ndege na miradi ya nishati ya umeme. 

Kabla ya kuzuru China, rais huyo wa Zambia alitembelea Ufaransa mwezi Juni na kukubaliana na rais Emmanuel Macron kuhusu utaratibu wa kupangilia upya namna ya kulipa deni lake. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.