Pata taarifa kuu

Zambia: Edgar Lungu anamtuhumu mrithi wake kwa kushindwa kuongoza

Nairobi – Rais wa zamani wa Zambia Edgar Lungu ametoa wito kwa raia kwenye taifa hilo kuitisha uchaguzi wa mapema, akimtuhumu mrithi wake Hakainde Hichilema, kwa kushindwa kuongoza nchi.

Kwa upande wake, msemaji wa serikali ya Zambia anasema Lungu aliongoza  nchi hiyo vibaya wakati wake
Kwa upande wake, msemaji wa serikali ya Zambia anasema Lungu aliongoza nchi hiyo vibaya wakati wake AFP PHOTO/CHIBALA ZULU-REUTERS/Rogan Ward
Matangazo ya kibiashara

Aidha Lungu pia anamtuhumu rais Hichilema kwa kushindwa kukabiliana na msambao wa maambukizo ya kipindupindu, ambao umesababisha vifo vya karibia watu 600 tangu mwezi Oktoba mwaka jana.

Wakati akizungumza na wanahabari, Lungu amewataka wapiga kura kushinikiza kufanyika kwa uchaguzi huo wa urais mapema.

Rais wa zamani wa  Zambia Edgar Lungu amemtuhumu mrithi wake kwa kushindwa kuongoza vyema
Rais wa zamani wa Zambia Edgar Lungu amemtuhumu mrithi wake kwa kushindwa kuongoza vyema © REUTERS/Rogan Ward

Kwa upande wake msemaji wa serikali Cornelius Mweetwa ametupilia mbali matamshi ya rais huyo wa zamani akitoa wito wa raia wa Zambia kumpa muda rais wa sasa ilikutekeleza agenda zake alizotoa wakati wa kampeni.

Aidha serikali imemtuhumu kiongozi huyo wa zamani kwa kuharibu uchumi wa nchi yake wakati wa kipindi chake cha miaka sita afisini.

Msemaji wa serikali amewataka wapiga kura kumpa muda rais Hichilema kutekeleza agenda zake
Msemaji wa serikali amewataka wapiga kura kumpa muda rais Hichilema kutekeleza agenda zake AP - Lewis Joly

Mwezi Oktoba mwaka uliopita, Lungu alitangaza kurejea tena katika ulingo wa kisiasa, hatua ambayo ilipelekea serikali kuwaondoa mafao yake.

Lungu alikuwa amestaafu kutoka kwa siasa mwaka wa 2021 baada ya kushindwa kutetea kiti chake katika uchaguzi mkuu wa urais.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.