Pata taarifa kuu
MVUTANO-DIPLOMASIA

Somalia: Puntland na Somaliland zakataa kufunga balozi ndogo za Ethiopia

Majimbo ya Somalia ya Puntland na Somaliland siku ya Ijumaa yamekataa kufungwa kwa balozi ndogo za Ethiopia katika ardhi zao, agizo lililotolewa siku moja kabla na serikali ya shirikisho ambayo inaishutumu Addis Ababa kwa "kuingilia mambo (yake) ya ndani".

Bandari ya Berbera huko Somaliland ndio kiini cha makubaliano kati ya Ethiopia na jamhuri hii ndogo iliyojitenga. (picha ya kielelezo)
Bandari ya Berbera huko Somaliland ndio kiini cha makubaliano kati ya Ethiopia na jamhuri hii ndogo iliyojitenga. (picha ya kielelezo) AFP - ED RAM
Matangazo ya kibiashara

Somalia siku ya Alhamisi iliagiza balozi wa Ethiopia kuondoka ndani ya saa 72 kwenye ardhi yake na kumrejesha nyumbani balozi wake mjini Addis Ababa kwa mashauriano. Mogadishu pia ilitangaza kufungwa "ndani ya wiki moja " balozi ndogo za Ethiopia katika mikoa ya kaskazini ya Puntland na Somaliland.

Serikali ya Puntland, ambayo ilitangaza uhuru wake mwaka 1998 na inadumisha mvutano na Mogadishu, imesema katika taarifa kwamba "uamuzi wa kufunga ubalozi mdogo huko Garowe (mji mkuu wa jimbo hilo) hauhusu Puntland.

Imeelezea uamuzi huu kutokana na kwamba "serikali ya shirikisho ya Somalia imefuta Katiba ambayo ilizingatia umoja wa kitaifa", siku chache baada ya kutangaza kwamba "haitambui tena taasisi za serikali ya shirikisho ya Somalia" kufuatia bunge kuidhinisha mpito hadi mfumo wa urais. Siku ya Jumatano, wajumbe kutoka Puntland walipokelewa katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia.

Jimbo lililojitenga la Somaliland, ambalo lilijitangazia uhuru wake kutoka kwa Somalia mwaka 1991 lakini halitambuliki na jumuiya ya kimataifa, pia lilikataa uamuzi wa Mogadishu, ambalo linasema haina mamlaka juu ya eneo lake.

"Ubalozi wa Ethiopia katika Jamhuri ya Somaliland haukufunguliwa awali kwa idhini ya Somalia na (...) kwa hivyo hautafungwa," Wizara ya Habari ya Somaliland imetangaza katika taarifa yake. "Ni uzembe na ni kinyume cha kidiplomasia kusema kwamba ubalozi wa nchi ambayo huna udhibiti unapaswa kufungwa," anaongeza.

Mamlaka ya Somaliland na Ethiopia waliibua hasira ya serikali ya Somalia kwa kutangaza Januari 1 kutiwa saini "itifaki ya mkataba" unaotoa ukodishaji wa kilomita 20 za ufuo wa Somaliland hadi Ethiopia kwa miaka 50. Mogadishu ilishutumu makubaliano "haramu", "ukiukwaji wa uhuru wake" sawa na "uchokozi". Mamlaka ya Somaliland ilidai kuwa badala ya njia hii ya kufikia bahari, Ethiopia itakuwa nchi ya kwanza kuwatambua rasmi.

Serikali ya Ethiopia hadi sasa imesema tu kwamba "itafanya tathmini ya kina kwa nia ya kuchukua msimamo kuhusu juhudi za Somaliland kupata kutambuliwa." Mogadishu imeondoa uwezekano wowote wa upatanishi na Ethiopia hadi Ethiopia itakapojiondoa kwenye makubaliano na Somaliland.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.