Pata taarifa kuu

Mogadishu yamfukuza balozi wa Ethiopia

Nairobi – Somalia imemfukuza balozi wa Ethiopia nchini humo Muktar Mohamed Ware kutokana na uhusiano baridi kati ya nchi hizo mbili za pembe ya pembe ya Afrika.

Uhusiano kati ya Ethiopia na Somalia uliingia doa mwezi Januari baada ya serikali ya Addis Ababa kuingia kwenye makubaliano na uongozi wa Somaliland ili kuiruhusu kufikia bahari na kujenga kituo cha jeshi.
Uhusiano kati ya Ethiopia na Somalia uliingia doa mwezi Januari baada ya serikali ya Addis Ababa kuingia kwenye makubaliano na uongozi wa Somaliland ili kuiruhusu kufikia bahari na kujenga kituo cha jeshi. © REUTERS/Feisal Omar
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja baada ya Waziri Mkuu Hamza Barre, kuongoza kikao cha Baraza la Mawaziri na ikakabuliwa kuwa kwa sababu ya madai ya Ethiopia kuingilia masuala ya ndani ya Somalia, Balozi wake aondoke Mogadishu kuanzia siku ya Alhamisi.

Kutokana na hatua hiyo, ubalozi mdogo wa Ethiopia mjini Hargeisa, katika jimbo la Somaliland na Garowe, katika jimbo la Puntland zitafungwa.

Hatua hii inakuja siku moja tu baada ya jimbo la Puntland, kutangaza ushirikiano mpya na Ethiopia, kufuatia hatua yake pia ya kuamua kujitawala yenyewe bila ya kushirikiana na uongozi wa Mogadishu.

Uhusiano kati ya Ethiopia na Somalia uliingia doa mwezi Januari baada ya serikali ya Addis Ababa kuingia kwenye makubaliano na uongozi wa Somaliland ili kuiruhusu kufikia bahari na kujenga kituo cha jeshi.

Somalia imekuwa ikisema hatua hii ni kinyume cha sheria na ni mpango wa Ethiopia, kuchukua sehemu ya nchi yake, na kuamua kumrudisha nyumbani balozi wake kutoka jijini Addis Ababa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.