Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-DEMOKRASIA

Uchaguzi wa rais wa Algeria wasogezwa mbele hadi Septemba 7, 2024

Algeria imetangaza siku ya Alhamisi kufanyika kwa uchaguzi wa urais "wa mapema" Septemba 7, 2024, miezi mitatu kabla ya tarehe iliyopangwa awali.

Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune mwaka 2019.
Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune mwaka 2019. © AFP
Matangazo ya kibiashara

"Iliamuliwa kuandaa uchaguzi wa mapema wa rais mnamo Septemba 7, 2024," imebainisha ofisi ya rais wa jamhuri katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa mwishoni mwa mkutano ulioongozwa na mkuu wa nchi Abdelamadjid Tebboune, mbele ya Waziri Mkuu wake , wakuu wa Mabunge mawili, Mkuu wa Majeshi na Rais wa Mahakama ya Katiba. "Baraza la uchaguzi litaitishwa mnamo Juni 8, 2024," imeongeza taarifa kwa vyombo vya habari.

Uchaguzi uliopita wa urais, ambao Bw. Tebboune alishinda kwa asilimia 58 ya kura na kukumbwa na kiwango kidogo cha ushiriki , ulifanyika Desemba 12, 2019. Alimrithi Abdelaziz Bouteflika, ambaye alilazimika kujiuzulu mwaka wa 2019 kwa shinikizo kutoka kwa jeshi na Hirak, vuguvugu la kiraia la maandamano. Alifariki mnamo Septemba 2021.

Akiwa amedhoofishwa sana na kiharusi kutoka mwaka 2013, Abdelaziz Bouteflika bado aligombea kwa muhula wa 4 mnamo mwaka 2014, na alijaribu kupata muhula wa tano mnamo mwaka 2019, na kusababisha wimbi la maandamano ambayo yalimsukuma kujiuzulu. Mbali na upinzani kwa mamlaka mpya ya Abdelaziz Bouteflika, Hirak iliongeza madai ya mageuzi ya kisiasa uhuru.

Muhula wa miaka mitano wa Bw. Tebboune ulipaswa kumalizika mwezi wa Desemba mwaka huu. Hakuna sababu imetolewa kueleza kufanyika mapema kwa uchaguzi ujao. Bw. Tebboune, 78, bado hajatangaza iwapo atawania muhula wa pili. Alilazwa hospitalini kwa miezi kadhaa nchini Ujerumani baada ya kuambukizwa UVIKO mwishoni mwa mwaka 2020.

Tangazo la mshangao

Katika ripoti iliyochapishwa mwezi Februari, shirika lisilo la kiserikali la Amnesty International lilithibitisha kwamba mamlaka ya Algeria iliendelea "kukandamiza haki za uhuru wa kujieleza na kukusanyika au kuandamana kwa amani", kwa "kulenga sauti za upinzani", miaka mitano baadaye maandamano ya Hirak ya kuunga mkono demokrasia. Uamuzi wa serikali ya Algeria kuwasilisha tarehe ya kupiga kura unaonekana kuwashangaza waangalizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.