Pata taarifa kuu

Uhusiano kati ya Algiers na Abu Dhabi unaendelea kuzorota

Ni mzozo wa kimya kimya ambao umeibuka tangu mwaka 2021 kati ya Algeria na Falme za Kiarabu, lakini ambao umechukua mkondo mbaya zaidi tangu msimu wa joto uliopita. Vyombo vya habari vya serikali vya Algeria vinaongeza idadi ya taarifa zinazoripoti mvutano huu.

Mohammed Ben Zayed Al Nahyan, Rais wa Falme za Kiarabu.
Mohammed Ben Zayed Al Nahyan, Rais wa Falme za Kiarabu. AFP - ABDULLA AL-NEYADI
Matangazo ya kibiashara

Ni vyombo vya habari vya ndani vilivyo karibu na serikali ya Algeria ambavyo mara nyingi vinaelezea kutoridhika kwa Algiers ambayo inazingatia kwamba Abu Dhabi inafanya kazi nyuma ya pazia dhidi ya masilahi ya Algeria. Abu Dhabi kwa hivyo ingekuwa moja ya nchi adimu kupiga kura dhidi ya kugombea kwa Algiers katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Pia angeishawishi India kupiga kura dhidi ya kuunganishwa kwa Algiers katika Brics.

Bila ya onyo, Falme za Kiarabu zilichukua vikwazo dhidi ya watu mashuhuri wa Algeria wanaochukuliwa kuwa maadui, na haiwapi tena visa. Wanaishutumu Algiers kwa kuwa na uadui kwa maslahi yao katika Afrika Kaskazini na  Kusini mwa Jangwa la Sahara, wakati Algiers inashutumu Abu Dhabi kwa kufanya kazi kwa pamoja na Israel na Morocco "kuyumbisha usalama wake wa taifa".

Hivi majuzi, redio ya taifa ya Algeria ilishutumu Falme za Kirabu kwa kufadhili Morocco kwa kiasi cha dola milioni 15 ili kudhoofisha uhusiano wake na nchi jirani za Sahel. Mwezi uliopita, Louisa Hanoune, katibu mkuu wa Chama cha Wafanyakazi ndiye ambaye alitangaza baada ya mkutano na Rais Tebboune kwamba "anafahamu sakata hiyo".

Kwa hakika, katika masuala ya kikanda na katika siasa za kijiografia, nchi hizo mbili zinakinzana: Algiers iko karibu na Uturuki, Qatar na Iran wakati Falme za Kiarabu ni washirika wa Israel na Morocco. Kuhusu suala la Libya, nchi hizo mbili pia zinakinzana: Abu Dhabi inamuunga mkono Marshal Haftar, kiongozi mwenye nguvu wa mashariki mwa Libya, huku Algiers ikiunga mkono Tripoli.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.