Pata taarifa kuu
BIASHARA-USHIRIKIANO

Algeria na Mauritania, wazinduzi miradi mipya ya kuimarisha ushirikiano wao

Marais wa Algeria na Mauritania wanaimarisha uhusiano kati ya nchi zao mbili: Abdelmadjid Tebboune na Mohamed Ould Ghazouani walizindua, Februari 22, 2024, vituo viwili vya mpaka na kutangaza uzinduzi wa mradi wa barabara kati ya Tindouf, nchini Algeria, na Zouerate, nchini Mauritania. Viongozi hao wawili pia waliweka jiwe la kwanza la eneo la biashara huria la siku zijazo. Hatua moja zaidi kuelekea ushirikiano wa kimkakati.

[Picha ya zamani] Picha ya skrini kutoka kwa video iliyochapishwa na huduma ya vyombo vya habari ya rais wa Algeria mnamo Desemba 28, 2021 inayomwonyesha Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune (kulia) akikutana na Rais wa Mauritania Mohamed Ould Ghazouani (kushoto) akizuru ikulu ya Mouradia Palace huko Algiers, mji mkuu.
[Picha ya zamani] Picha ya skrini kutoka kwa video iliyochapishwa na huduma ya vyombo vya habari ya rais wa Algeria mnamo Desemba 28, 2021 inayomwonyesha Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune (kulia) akikutana na Rais wa Mauritania Mohamed Ould Ghazouani (kushoto) akizuru ikulu ya Mouradia Palace huko Algiers, mji mkuu. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Wakuu wa nchi za Algeria na Mauritania siku ya Alhamisi hii walizuru eneo la mpaka wa nchi zao mbili. Walizindua vituo viwili vya kudumu vya mpaka, hivyo kutangaza uzinduzi wa mradi wa barabara inayounganisha Tindouf nchini Algeria hadi Zouerate nchini Mauritania.

Abdelmadjid Tebboune na Mohamed Ould Ghazouani pia waliweka jiwe la kwanza la eneo la biashara huria lililo karibu na kituo cha mpaka upande wa Algeria. Hatua moja zaidi ya kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili zinazohusishwa na "ushirikiano wa kimkakati".

Kipindi cha kuanzia kinatolewa kwa ajili ya kuanza kazi. Barabara inayounganisha Tindouf na Zouerate ina urefu wa kilomita 840. Itawawezesha wafanyabiashara na wawekezaji wa Algeria kufikia masoko ya Afrika, kupitia Mauritania.

Kwa mujibu wa Shirika la Vyombo vya Habari la Algeria (APS), kituo cha mpakani kwa upande wa Algeria kina huduma zote muhimu na kinapaswa "kuanzisha mfumo wa kiuchumi" kati ya nchi hizo mbili.

Kuhusu eneo huria, litaunda kiunganishi katika suala la mabadilishano ya kibiashara na kiviwanda kati ya Algeria na nchi za Afrika Magharibi, ambapo kiasi cha uagizaji na mauzo ya nje kinarekodi maendeleo makubwa.

Algeria chini ya Rais Tebboune imesonga mbele kuelekea sera ya usafirishaji isiyo ya hidrokaboni. Mkuu wa nchi ya Algeria jana alisisitiza haja ya kuimarisha uwekezaji na biashara kati ya mataifa hayo mawili. Alitoa mfano wa sukari na mafuta ambayo Algeria inaweza kuuza Mauritania katika siku zijazo.

Mbali na hayo, kuna miradi mitano ya eneo huria ambayo Algeria inataka kuanzisha kwenye mpaka na majirani zake. Laiki miradi pamoja na Mauritania ndiyo ya kwanza ambayo itaanza kutekelezwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.