Pata taarifa kuu

Tunisia: Watu 35 wajeruhiwa katika mlipuko katika ghala la kampuni ya mafuta

Watu 35 wamejeruhiwa, wanne kati yao wako katika hali mbaya, katika mlipuko uliotokea siku ya Alhamisi katika ghala la kampuni ya mafuta ya umma katika vitongoji vya kusini mwa Tunis, kikosi cha polisi jamii kimesema.

Watu wanne waliojeruhiwa wako katika uangalizi maalum kufuatia moto katika ghala la gesi la kampuni ya kitaifa ya usambazaji mafuta ya Agil (...) huko Radès.
Watu wanne waliojeruhiwa wako katika uangalizi maalum kufuatia moto katika ghala la gesi la kampuni ya kitaifa ya usambazaji mafuta ya Agil (...) huko Radès. © AFP
Matangazo ya kibiashara

"Saa 12:15 asubuhi (saa za hapa), uvujaji wa gesi ulisababisha mlipuko wa chupa za gesi (kwa matumizi ya nyumbani) katika majengo ya kampuni ya utumiaji na usambazaji wa gesi katika eneo la mafuta huko Radès," msemaji wa kikosi cha polisi jamii, Moez Triaa, ameliamia shirika la habari la AFP. Majeruhi, wafanyakazi wote wa kampuni hii, wamepata majeraha madogo madogo na makubwa ya viwango vya kwanza na vya pili na wamelazwa hospitalini. Wanne kati yao wako katika uangalizi maalum, ameongeza Bw. Triaa.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Wizara ya Viwanda, Migodi na Nishati imebaini kwa upande wake kwamba "moto uliozuka katika ghala la gesi la kampuni ya kitaifa ya usambazaji mafuta ya AGIL (... ) huko Radès, umedhibitiwa. Uchunguzi umefunguliwa ili kubaini "mazingira ya tukio hili", imeongeza wizara bila kutaja kiwango cha uharibifu.

AGIL, kampuni kubwa zaidi ya usambazaji wa mafuta nchini Tunisia, inauza bidhaa za petroli. Ina mtandao wa zaidi ya vituo 250 vya huduma nchini kote.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.