Pata taarifa kuu
USALAMA-MARIDHIANO

Mali: Viongozi sita wa JNIM na waasi wa Tuareg walengwa na vikwazo vya kifedha

Agizo kutoka kwa Wizara ya Uchumi la tarehe 8 Machi linazuiwa kwa miezi sita inayoweza kurejeshwa "mali" ya Iyad Ag Ghaly, mkuu wa kundi clinalodai kutetea Uislamu na Waislamu (GSIM au JNIM), na Amadou Kouffa, mkuu wa Katiba Macina, katika muungano huo.

Operesheni hii inafanyika wakati kaskazini mwa Mali imekuwa eneo la mapigano tangu mwishoni mwa mwezi wa Agosti kutoka kwa makundi yenye silaha ya Tuareg yanayotaka kujitenga na kuongezeka kwa mashambulizi ya wanajihadi dhidi ya jeshi la Mali.
Operesheni hii inafanyika wakati kaskazini mwa Mali imekuwa eneo la mapigano tangu mwishoni mwa mwezi wa Agosti kutoka kwa makundi yenye silaha ya Tuareg yanayotaka kujitenga na kuongezeka kwa mashambulizi ya wanajihadi dhidi ya jeshi la Mali. © AFP - Kenzo Tribouillard
Matangazo ya kibiashara

Watu wengine wanne wanaolengwa na vikwazo hivi ni Alghabass Ag Intalla, Bilal Ag Acherif, Fahad Ag Almahmoud na Achafagui Ag Bouhada, viongozi wa waasi wa Tuareg ambao walichukua tena silaha dhidi ya serikali ya Mali mwaka 2023. Agizo hilo linawawasilisha kama wanachama au washirika wa JNIM. Sababu halisi za kuzuia mali zao haziko wazi.

Wote wanaelezewa kuwa raia wa Mali na kwa kawaida wanaishi Mali, isipokuwa Bilal Ag Acherif, raia wa Mali lakini mzaliwa wa Burkina Faso. Mahali pa makazi yake ya kawaida haijaonyeshwa. Wote wanatuhumiwa kwa "vitendo vya ugaidi", "ufadhili wa kigaidi", "mashambulizi dhidi ya uadilifu wa eneo" au "kujiunga na kundi la uhalifu".

Wanaume hao sita, ambao wana historia ndefu ya kuhusika kwa mashambulizi dhidi ya serikali kuu, walikuwa kwenye orodha ya watu wanaolengwa na kufunguliwa kwa uchunguzi wa mahakama uliotangazwa Novemba 28 na mahakama nchini Mali kwa sababu sawa. Tangu mwaka wa 2012, Mali imekuwa ikikumbwa na vitendo vya makundi yenye mafungamano na Al-Qaeda na kundi la Islamic State, ghasia zinazofanywa na makundi yaliyotangaza kujilinda na ujambazi.

Mgogoro wa usalama unaambatana na mzozo mkubwa wa kibinadamu na kisiasa. Nchi hiyo inaongozwa na wanajeshi kufuatia mapinduzi mawili, ya mwaka wa 2020 na 2021. Waasi wanaotaka kujitawala wengi wao kutoka jamii ya Watuareg ambao walitia saini makubaliano ya amani mwaka wa 2025 walianzisha tena uhasama kaskazini mwaka jana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.