Pata taarifa kuu
MAUAJI-HAKI

DRC: Malalamiko yawasilishwa dhidi ya Serikali baada ya mauaji ya Djugu, Ituri

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wiki tatu baada ya mauaji ya raia kumi na watano huko Djugu, katika mkoa wa Ituri, familia za wahanga pamoja na shirika la Ente linaloleta pamoja jamii ya Hema, wamewasilisha malalamiko mbele ya mahakama.

Djugu, DRC, imeendelea kukumbwa na vurugu tangu mwaka 2017 (Picha ya Kielelezo).
Djugu, DRC, imeendelea kukumbwa na vurugu tangu mwaka 2017 (Picha ya Kielelezo). AFP - ALEXIS HUGUET
Matangazo ya kibiashara

Kwa hivyo malalamiko yaliwasilishwa dhidi ya wanamgambo wenye silaha, Ushirika wa Maendeleo ya Kongo (CODECO), wanaodaiwa kutekeleza mauaji hayo. Malalamiko pia dhidi ya serikali kwa sababu mauaji hayo yalitekelezwa chini ya kilomita 2 kutoka kituo cha jeshi.

Raia hawawezi kuvumilia tena, anaelezea Jean Bosco Kisoké, kiongozi wa shirika la vijana kutoka Jumuiya ya Hema, aliyehojiwa na RFI: “Tunachotaka ni haki itendeke. Rais amekuwa hapa kwa muda mrefu - ilikuwa Julai 2019 - kuelezea kile kilichotokea kama jaribio la mauaji ya kimbari. Baada ya hapo hakuna kilichofanyika. Ripoti za haki za binadamu za Umoja wa Mataifa zilihitimu, mwaka 2020, uhalifu wa kivita na uhalifu wa mauaji ya halaiki, kile CODECO inafanya hapa,  Ituri. Hakuna kilichofanyika.

"Tahadhari ya serikali inalenga zaidi mashariki"

“Mbele ya Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa, CODECO na M23 hawakujumuishwa katika mchakato wa amani kwa sababu walichukua silaha dhidi ya Jamhuri lakini utaona kwamba jinsi tunavyowachukulia M23, ni tofauti na CODECO.

"Tahadhari ya serikali inalenga zaidi mashariki mwa nchi, mkoa wa Kivu Kaskazini," anaendelea Jean Bosco Kisoké. Tunataka umakini huu kutoka kwa serikali ya Kongo uwe sawa hapa, kwa mkoa wa Ituri, kwa sababu hatuwezi kuvumilia tena. Tumehesabu vifo vingi. Bado tumechanganyikiwa na tunashangaa tukijiuliza serikali iko wapi. Hata hivyo, serikali bila raia, hakuna serikali haipo. Raia wanaouawa mara kwa mara hulipa ushuru wa serikali na tunashiriki katika majukumu yote ya serikali lakini, ili kutoa ulinzi kwa raiai, ni shida tupu. Tunashangaa jukumu la Serikali ni nini hasa. Raia hao walitekwa chini ya kilomita 2 kutoka kwa vikosi vya serikali. Hii haikubaliki! "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.