Pata taarifa kuu

DRC: Jeshi la serikali lazidi kuimarisha vita vikali dhidi ya waasi wa M23

Nairobi – Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, jana kuliripotiwa makabiliano makali ya silaha nzito kati ya wanajeshi wa serikali FARDC na waasi wa M 23 wanaodaiwa kuungwa mkono na jeshi la Rwanda karibu na miji ya Sake na Shasha iliyoko umbali wa kilomita 27 na 40 kusini mwa mji wa Goma.

Mapigano yanafanyika kwenye maeneo kadhaa ya waasi yaliyo juu ya kilima cha Ndumba, karibu na mji wa Shasha, katika eneo la Mufuni Shanga.
Mapigano yanafanyika kwenye maeneo kadhaa ya waasi yaliyo juu ya kilima cha Ndumba, karibu na mji wa Shasha, katika eneo la Mufuni Shanga. AFP - ALEXIS HUGUET
Matangazo ya kibiashara

Vyanzo vilivyothibitishwa na mashirika ya kiraia vinasema kuwa hadi saa sita mchana jana Jumapili, milio ya silaha nzito ilikuwa ikisikika karibu na jiji la Sake, ambapo mapigano hayo makali yanavihusisha vikosi vya serikali dhidi ya vile vya waasi wa M23.

Mapigano yanafanyika kwenye maeneo kadhaa ya waasi yaliyo juu ya kilima cha Ndumba, karibu na mji wa Shasha, katika eneo la Mufuni Shanga.

Kwa mujibu wa vyanzo hivyohivyo, Mlima Ndumba ndio kitovu cha kwanza katika operesheni ambayo inaruhusu waasi kudhibiti ngome zao za nyuma kutoka Mushaki, Kilolirwe hadi Mweso, kupitia Kitchanga.

Mapigano mengine yalianza tena Jumapili hii mwendo wa saa 3 asubuhi kwenye maeneo tofauti ya eneo la Masisi, kati ya Wazalendo na waasi. Hii ni hasa kwenye barabara za Kimoka, kwenye lango la kijiji cha Malehe, Kisheke nyuma ya kituo cha MONUSCO na kule Tingi kuelekea kijiji cha Lutobogo.

Vyanzo vya mashirika ya kiraia katika eneo la Masisi vinabainisha kuwa kwa sasa ni vigumu kufanya tathmini ya mapigano haya kutokana na kutofikiwa kwa maeneo ya mapigano.

Wakati hiuo huo Utulivu ulirejea Jumapili hii, Februari 25 jioni karibu na mji wa Sake na kwenye mhimili wa Shasha-Bweremana, kusini mwa mji wa Goma, katika eneo la Masisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.