Pata taarifa kuu

Addis Ababa: Mkutano wa 37 wa wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika kuanza Jumamosi

Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika utafanyika kuanzia Februari 17 hadi 18 mjini Addis Ababa, nchini Ethiopia.

Makao makuu ya Umoja wa Afrika, Addis Ababa.
Makao makuu ya Umoja wa Afrika, Addis Ababa. AFP - MICHELE SPATARI
Matangazo ya kibiashara

 

Mkutano huu, ambao unawaleta pamoja wakuu wa nchi na serikali za Afrika, unaandaliwa katikati ya hali ya migogoro mingi ya kisiasa na kiusalama inayotikisa bara la Afrika.

Lakini tayari mwanzoni mwa wiki hii, baraza kuu la Umoja wa Afrika pamoja na mawaziri wa mambo ya nje walianza mkutano huo.

Mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat, ambaye muhula wake unamalizika mwaka ujao, anasema ana wasiwasi kuhusu hatima ya bara lililoathiriwa na mapinduzi na migogoro kadhaa.

Ndio maana baadhi ya wadau hawafichi mshangao wao wa kutoona mivutano mingi ambayo imekuwa ikitikisa bara la Afrika kwa miezi kadhaa ikiendana na ajenda.

Hata hivyo, upande wa DRC unatarajia kushughulikia suala la usalama na uvamizi wa eneo lake na Rwanda kupitia waasi wa M23.

Hakika, mikutano midogo midogo na mijadala imepangwa sambamba juu ya mzozo wa Kivu Kaskazini.

Hata hivyo, ajenda isiyo ya mwisho ya mkutano huo inapanga kuzingatia mageuzi ya muundo wa umoja huo. Na ni ndani ya mfumo huu ambapo Rais wa Rwanda Paul Kagame, ambaye ameteuliwa kuongoza mchakato wa mageuzi ya kitaasisi ya Umoja wa Afrika (AU), atawasilisha ripoti ya mwisho kuhusu mageuzi ya taasisi hiyo.

Mambo mengine katika ajenda hiyo ni pamoja na suala la ushirikiano wa pande nyingi, lakini pia masuala yanayohusu uchumi na biashara, ikiwa ni pamoja na kuongeza kasi ya utekelezaji wa Eneo Huria la Biashara ya Bara la Afrika (ZLECAF).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.