Pata taarifa kuu

New York: Mkutano wa pande tatu kati ya viongozi wa Umoja wa Mataifa, AU na EU

Mjini New York, zaidi ya viongozi 140 wanatarajiwa kwa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa utakaoanza wiki ijayo. Kabla ya mkutano huu, mkutano ambao haujafanyika kwa miaka minne umeitishwa Jumapili siku ya Septemba 17 kati ya viongozi wake: pande tatu kati ya Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika (AU) na Umoja wa Ulaya (EU).

Rais wa Tume ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, wakati wa mkutano na waandishi wa habari mwaka 2019.
Rais wa Tume ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, wakati wa mkutano na waandishi wa habari mwaka 2019. AFP - TONY KARUMBA
Matangazo ya kibiashara

Ikiwa maafisa wa taasisi hizo tatu watafanya kazi pamoja karibu kila siku, viongozi wao hawajakaa meza moja kwa miaka minne: Antonio Guterres wa Umoja wa Mataifa, rais wa Tume ya AU, Moussa Faki Mahamat, na Kamishna wa Amani na Usalama Bankole Adeoye na kwa EU, Rais wa Tume ya Ulaya, Charles Michel, na Waziri wake wa Mambo ya Nje, Josep Borrell.

Watatumia dakika 90 pamoja, isipokuwa katika ratiba ya Antonio Guterres ambaye ana mikutano ya nchi mbili kila baada ya dakika 20 wiki hii, anabainisha mwandishi wetu mjini New York, Carrie Nooten. Watajadili ugombea wa Afrika kwa G20, hali katika Sahel, Pembe ya Afrika au Maziwa Makuu. Lakini pia uhamiaji, pamoja na mshikamano muhimu kati ya Ulaya na Afrika.

Umoja wa Ulaya unaweza pia kutuma ishara kali ya kisiasa, ikiwa itajitangaza rasmi kwa ajili ya mageuzi ya usanifu wa fedha wa kimataifa, na kupendekeza kuingia na ombi la nchi za Afrika katika mwelekeo huu. Hatimaye, suala jingine kubwa linapaswa kutajwa: ufadhili wa shughuli za amani za Afrika, moja kwa moja kutoka kwa bajeti ya kawaida ya Umoja wa Mataifa. Hili ni pendekezo lililoshinikizwa na Ghana, ambayo kwa sasa iko katika Baraza la Usalama. China na Marekani wananajikita kuzuia mambo ingawa wanajua vyema kwamba Umoja wa Mataifa hautakubali mradi tu ujumbe wa AU hauendani na vigezo kulazimisha vya Umoja wa Mataifa.

Lengo la ushawishi kwa EU

Madhumuni mengine wakati wa mkutano huu wa pande tatu ni kujibu matarajio ya Kusini mpya, ambayo pia inaitwa "Kusini ya kimataifa". Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya wana maslahi gani mbele ya China, ambayo inaendeleza vipaji vyake kimataifa? 

“Umoja wa Ulaya ambao ulikuwa umewekeza fedha nyingi baada tu ya uhuru miaka ya 1960 katika kuhitimisha mikataba na nchi za Kusini na ambao kwa namna fulani ushawishi wake unapungua.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.