Pata taarifa kuu

Zaidi ya wahamiaji 1,300 kutoka Tunisia walikufa au kutoweka mwaka 2023

Zaidi ya wahamiaji 1,300 walioondoka kwenye pwani ya Tunisia kujaribu kuingia Ulaya kinyume cha sheria waliangamia baharini mwaka 2023, shirika la Haki za Kiuchumi na Kijamii la Tunisia, shirika lisilo la kiserikali ya Tunisia linalohusika na masuala ya uhamiaji, limetangaza siku ya Jumanne.

Boti ya wahamiaji kutoka pwani ya kaskazini mwa nchi, karibu na Tripoli. Picha iliyotolewa na jeshi la Lebanon mnamo Desemba 31, 2022.
Boti ya wahamiaji kutoka pwani ya kaskazini mwa nchi, karibu na Tripoli. Picha iliyotolewa na jeshi la Lebanon mnamo Desemba 31, 2022. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

 

Kwa jumla "watu 1,313 walikufa au kutoweka katika pwani ya Tunisia, idadi ambayo haijawahi kuripotiwa nchini Tunisia," Islem Ghaarbi, mtaalam wa uhamiaji katika FTDES, ameviambia vyombo vya habari.

Mtaalamu huyo, ambaye ametaja kwamba angalau thuluthi mbili ya wahanga ni Kusini mwa Jangwa la Sahara, amesisitiza kwamba idadi hiyo “ni sawa na takriban nusu ya vifo na watu kutoweka katika Bahari ya Mediterania” mwaka wa 2023. Zaidi ya watu 2,498 walikufa au kutoweka mwaka 2023 katikati mwa Mediterania, asilimia 75 zaidi ya mwaka uliopita, kulingana na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM).

Kuondoka kwa raia wa Kusini mwa Jangwa la Sahara kuliongezeka kwa kasi nchini Tunisia baada ya hotuba ya Februari 2023 ya Rais Kais Saied, akilaani kuwasili kwa "makundi ya wahamiaji haramu" ambayo aliwataja kama tishio la idadi ya watu kwa nchi yake.

 

Kulingana na ripoti ya Shirika la Kupambana na Mateso Duniani (OMCT) iliyochapishwa Desemba mwaka jana, wahamiaji, wakimbizi na wanaotafuta hifadhi nchini Tunisia wanakabiliwa na "vurugu za kila siku za kitaasisi", "kukamatwa kiholela", "kuhamishwa kwa nguvu" na "kufukuzwa kinyume cha sheria" kuelekea mipakani na Libya na Algeria.

Wiki iliyopita, wakimbizi 13 wa Sudan walikufa na wengine 27 kutoweka baada ya boti yao kuzama siku ya Alhamisi kutoka pwani karibu na Sfax (katikati-mashariki) ili kujaribu kuvuka Bahari ya Mediterania hadi Italia, ambayo pwani zake za karibu ziko umbali wa chini ya kilomita 150.

Hali mbaya ya kiuchumi nchini Tunisia huku ukuaji ukikadiriwa kuwa 1.2% kwa mwaka 2023 (nusu ya mwaka 2022) na ukosefu wa ajira kwa vijana kwa 38%, pia ni sababu muhimu kwa raia wengi wa Tunisia kutoroka nchi hiyo na kukimbilia Ulaya. Mnamo mwaka 2023, waliwakilisha nchi ya pili kwa wahamiaji haramu walioingia nchini Italia (kwa idadi ya watu 17,304) nyuma kidogo ya Waguinea (18,204), kulingana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Italia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.