Pata taarifa kuu

Comoro: Mahakama ya Juu yaidhinisha ushindi wa Azali Assoumani

Mahakama ya Juu zaidi nchini Comoro imeidhinisha leo Jumatano ushindi wa rais anayemaliza muda wake Azali Assoumani katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais uliopingwa na upinzani. 

Aliyekuwa kiongozi wa mapinduzi Azali Assoumani akisherehekea pamoja na wafuasi wake ushindi wake katika makao Makuu ya chama chake huko Moroni Januari 16, 2024.
Aliyekuwa kiongozi wa mapinduzi Azali Assoumani akisherehekea pamoja na wafuasi wake ushindi wake katika makao Makuu ya chama chake huko Moroni Januari 16, 2024. AFP - OLYMPIA DE MAISMONT
Matangazo ya kibiashara

 

Kutangazwa kwa matokeo ya muda wiki iliyopita kulifuatiwa na mapigano katika mji mkuu. "Kuna sababu ya kumtangaza kuwa amechaguliwa katika duru ya kwanza," imetangaza mahakama ya juu zaidi ya visiwa vya Bahari ya Hindi, ikibainisha kuwa "maombi ya kubatilishwa kwa uchaguzi wa urais yametangazwa kuwa hayakubaliki."

Rais anayemaliza muda wake wa Comoro, Azali Assoumani, alitangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais siku ya Jumanne Januari 16, katika duru ya kwanza iliyofanyika Jumapili Januari 14, 2024 katika visiwa vya Bahari ya Hindi, huku upinzani ukilaani udanganyifu katika uchaguzi.

 

"Washindani wangu lazima wafuate njia za kisheria, lazima wawe waadilifu," alisema mwanajeshi huyo wa zamani, 65, kutoka makao makuu ya chama chake cha kisiasa katika mji mkuu Moroni, baada ya Tume Hur ya Uchaguzi kumtangazwa mshindi kwa asilimia 62.97 ya kura.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.